Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa, safari za treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza zitaanza tena kuanzia Desemba 07, 2012 kwa siku za Jumanne na Ijumaa muda wa kuondoka katika Stesheni ya Dar utakuwa saa 8:30 mchana badala ya saa 11:00 jioni.
Hivyo basi , Mwananchi yeyote anayetaka kusafiri kwenda Mwanza anaweza kununua tiketi yake wakati wowote katika Stesheni iliyo karibu naye. Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake!
.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Novemba 29, 2012
mbona suala na madaraja ya tiketi hawasemi?! Awali treni toka Dar ilikuwa na 3rd class tu. Je na 2nd itakuwepo.
ReplyDeleteSafari za treni zinanikumbusha miaka ya 80 nilipokuwa sekondari nikitumia warrant. Usafiri salama kuliko basi tatizo waweza kutumia siku 5 kwa safari ya masaa 24!