Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia
abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa, safari
za treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Bara kuanzia Desemba 4, 2012
zitakuwa zikiondoka saa 8:30 mchana kila ya siku ya Jumanne na Ijumaa. badala
ya saa 11:00 jioni hii inatokana na sababu za kiutawala ikiwemo kutoa nafasi ya
uratibu wa huduma mpya ya treni ya jiji la Dar es Salaam ilioanza Oktoba 29,
2012. Hata hivyo kwa treni kutoka Kigoma na Mpanda muda wa kuondoka Katika stesheni hizo utabaki kama ulivyo katika
ratiba ya sasa.
Tafadhali
atakayesoma taarifa hii amuarifu na mwenzake.
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote
utakaojitokeza.
Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi
Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Novemba 24, 2012



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...