Mkurugenzi
Mtendaji wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) Ndg. Sadick
Gogo akikabidhi baadhi ya Vifaa Tiba vyenye thamani ya TZS 5 Milioni kwa
Muwakilishi wa Taasisi ya Alhalaqul-Islam inayoshughulika na kutoa huduma za
Usaidizi katika Hospital Mbali Mbali katika Mikoa tisa nchi. Anayeshuhudia ni
Ndg . Sajid Iqbar Mwakilishi wa katika Kanda ya Afrika kutoka taasisi Rafiki ya
Kijamii ya Halping Hand for Relief and
Development ya Marekani.
Wawakilishi
wa Taasisi ya Ahlaqul -Islam wakiwa pamoja na Mwakilishi wa Helping Hand na
Wanyeji wao wa Taasisi ya Wanajumuia ya Wanataaluma wa Kiislam Tanzania Wakati
wa Makabidhiano ya vifaa tiba mbali mbali.
Mwenyekiti
wa Halmashauli ya Nzega Mh. Patrick Mbozu pamoja na Mbuge wa Jimbo la Bukene Mh.
Selemani Zedi wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Helping Hand
for Relief and Development pamoja na TAMPRO Kuboresha huduma za Afya katika
Halmashauri ya Nzega hususani Jimbo la Bukene.
Mbunge
wa Jimbo la Bukene Mh. Selemani Zedi akifafanua Changamoto na Mafanikio ya
Huduma ya Afya katika Halmashauli ya Nzega pamoja na Jimbo la Bukene kwa ofisa
mtendaji wa Helping Hand for Relief and Development Africa mbele ya Madiwani wa
Halmashauri ya Nzega. Pembeni kulia ni Ndg. Mohamed Kamilagwa, Mkuu wa Idara ya
Biashara na Maendeleo ya Jamii ya Jumuia ya wanataaluma wa Kiislam Tanzania
(TAMPRO) Makao Makuu.
Mbunge
wa Bukene Mh. Zedi Selemani akipokea baadhi ya vifaa tiba vya awali vyenye thamani
ya Zaidi TZS 30 Milioni kutoka kwa Muwakilishi wa Africa wa taasisi rafiki ya
Jumuia ya wanataaluma wa Kiislam (TAMPRO),
Helping Hand for Relief and Development ya Marekani Ndg Sajid Iqbar.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...