Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Mh. Thabo Mbeki (pichani) anatarajiwa kuhudhuria mkutano utakaojadili maswala ya uongozi Afrika jijini
Dar es Salaam kesho asubuhi.
Mkutano huo uliotayarishwa na UONGOZI Institute kwa
kushirikiana na Thabo Mbeki Foundation unahusisha wadau mbalimbali muhimu
watakaojadiliana kwa uwazi kuhusu wajibu wa uongozi na mustakabali wa bara la
Afrika.
“Hatuna nia ya kujenga dhana ya uongozi kwa bara la
Afrika, lakini majadiliano ya uwazi ya uongozi unaotakiwa kushughulikia
changamoto za maendeleo katika bara hili ni muhimu,” alisema Afisa Mtendaji
Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja jana katika taarifa.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, mazungumzo hayo yanalenga
kwenda mbali zaidi ya kuangalia changamoto zinazoikabili Afrika pamoja na
kukosoa uongozi lakini hasa kuangalia maswala yanayohusu aina ya viongozi
wanaotakiwa pamoja na matayarisho yanayohitajika ili kupata viongozi hao wenye
uwezo na mbinu za kuwawezesha kuongoza.
“Ni muhimu kwa Afrika kuwa na viongozi wenye uwezo
wa kukabiliana na changamoto za leo na kuwezesha bara hili kusonga mbele,”
alisema Prof. Masanja.
Mazungumzo hayo pia yatajadili uwezo wa viongozi
kutekeleza maswala mbalimbali kwa nyenzo na raslimali walizonazo, hali ya
taasisi na kama mazingira ya ndani na nje ya bara la Afrika yanasaidia au
kuzuia viongozi katika bara hilo kufanikisha malengo yao.
UONGOZI Institute hutayarisha mikutano kama hiyo na
kuwakutanisha viongozi kwa lengo la kujadili mada mbalimbali ili kufikia
malengo ya maendeleo endelevu Afrika.


Rais Mstaafu Mbeki tuna wezaje kusikia mkutano huu kuhusu uongozi kwenye bara la Afrika?Mara kwa mara tuna soma habari za mikutano lakini hakuna details.Je mkutano huu uta patikana kwenye youtube, Asante.
ReplyDelete