Wachezaji wa Toto wakiwa wamebeba kocha wao Athumani Bilal kwa furaha ya ushindi  wao wa bao 1-0 leo dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa jijini Dar
Na Mahmoud Zubeiry
BAO pekee la Mussa Said Kimbu dakika ya 73, leo limeizamisha Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Kimbu alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Mganda, Mohamed Jingo tena akipitisha mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert Mweta.
 
Simba hawakucheza vizuri kama timu leo, ila kwa mchezaji mmoja mmoja, karibu kila mchezaji alicheza vizuri na Emanuel Okwi ndiye aliyekuwa akiisumbua zaidi ngome ya Toto.
 
Katika michezo mingine ya ligi hiyo, Azam imefungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
 
Kwa matokeo hayo, Yanga inazidi kujinafasi kileleni kwa pointi zake 26, baada ya kucheza mechi 12 na kesho itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
 
Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.
 
Simba SC: Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto/Edward Christopher, Mrisho Ngassa/Haruna Chanongo, Felix Sunzu na Emanuel Okwi. 
 
Toto; Erick Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo/Robert Magadula, Evarist Maganga, Peter Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita/James Magafu, Kheri Mohamed/Mohamed Hussein, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Said. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera mgambo na Toto,hizi timu ndogo ndogo zinapoleta upinzani kwa timu kubwa ndipo ligi yetu inapokuwa na nguvu na kupendeza,tunaweza kupata timu bora ya taifa. Na nyie TFF mwambie huyo kocha wa Stars aangalie wachezaji kwenye hizi klabu ndogo ndogo,wamo.Mechi na Harambee stars ndiyo ilikuwa sehemu nzuri ya kujaribisha vijana wapya siyo kujaza SIMBA,AZAM na YANGA.Anahitaji kujenga timu ya baadae.

    David V

    ReplyDelete
  2. Mbebeni Kocha mzawa kamfunga kocha wa Kigeni tee teeeh eeeeeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  3. Simba SC ni Kigogo wa Rushwa!

    Ndio maana akikutana na mawe anachemka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...