Kwa zaidi ya miaka kumi biashara kati ya Africa na ulimwengu kwa ujumla imekua sana, wakati ambapo biashara kati ya Africa na nchi za Gulf Cooperation Council(GCC) imekua kwa asilimia 170. 

Mabadiliko yaliyozikumba nchi za Africa kutoka kwenye nchi tegemezi na kuelekea kwenye nchi za kibiashara, na uhusiano uliopo kati ya nchi za Africa na Mashariki ya Kati, imeuweka uchumi unaofuata sheria za kiIslam ktk nafasi muhimu ya kuandaa mazingira ya biashara kati ya Africa na nchi za Mashariki ya Kati

Umuhimu huo unaongezeka zaidi kwa sababu ya uhusiano mkubwa uliopo kati ya uchumi unaofuta sheria za kiIslam, biashara (real economic activity) na vyanzo vilivyopo ambavyo vinatoa mwanya wa biashara ktk nyanja muhimu kama vile Small and Medium Enterprises (SMEs). 

Hamu kubwa  ya wajasirimali wa Mashariki ya kati ktk biashara kama za kilimo, kununua ardhi na viwanda, kunategemewa kukuza kwa kiasi kikubwa uchumi wa bara la Africa.

Akizungumza kabla ya kikao mkurugenzi wa Islamic Banking Summit (IBSA) ndugu David McLean alinukuliwa akisema ‘kutokana na  mabadiliko ya baadhi ya sheria ktk soko la Africa, Africa imejipanga ktk nafasi ya tatu kwenye orodha ya uchumi unaokua kwa kasi duniani baada ya Mashariki ya Kati na nchi za Asia’. 

Alisisitiza kwamba ni kwa sababu kama hizo ndio zimetufanya tukutane kwenye kikao hichi cha the Islamic Banking Summit (IBSA 2012) kama hatua muhimu ambazo zitashughulikia malengo yaliyowekwa na World Islamic Banking Conference (WIBC).

 Kikao hicho kinachojulikana kama the Islamic Banking Summit kinategemewa kufanyika nchini Djibouti kwa mda wa siku mbili tarehe 6-7 mwezi wa kumi na moja mwaka 2012 kwa ajili ya kujadili fursa na changamoto zilizopo ktk uchumi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. UISLAMU UNAFUNDISHA KWAMBA MWENYEZI MUNGU YAANI ALLAH NDIYE ALIYEMUUMBA BINADAMU, NA KUPITIA DINI YAKE YA KWELI AMBAYO NI UISLAMU (MAANA YAKE KUJISALIMISHA KWA ALLAH NA KUFUATA KANUNI ZAKE ZOTE) NDIPO MAFANIKIO HUPATIKANA.
    BENKI NA UCHUMI WA KIISLAMU NI USHAHIDI MWENGINE WA KUTHIBITISHA MAFUNZO HAYO. LAITI BINADAMU TUTAFUATA MAFUNZO KAMILI YA UISLAMU, BILA KUJALI ITIKADI ZETU, MAISHA YETU YATAFANIKIWA ZAIDI.NDIYO MAANA NCHI ZA MAGHARIBI ZIMELISHTUKIA HILO, NA ZIMEANZA KUKIMBILIA KATIKA KUFUATA UCHUMI WA KIISLAMU.
    ALLAH AKBAR

    ReplyDelete
  2. I,for one,I hate mixing Religion with Business or Politics!Biashara misingi yake ni ile ile,iwe nchi za Kibepari au za Kijamaa au Kikomunisti au za Ki-Liberali!The Profit-Motive is the drive,nothing else,asikudanganye mtu Kaka!Ukibisha,hebu endesha biashara yako kwa hasara,uniambie!eti unatoa msaada,au wewe mtu mkarimu sana,biashara haina urafiki na mtu!Ukichanganya Dini na Siasa ndiyo kabisa,sawa,na kuzima moto kwa mafuta ya petroli!wenyewe mnajionea machafuko yasiyo kwisha sehemu mbalimbali duniani!Tuache kudanganyana jamani!Business shall always be for profit!How much profit?hapo ndio watu wanapo tofautiana!ushanfahamu!

    ReplyDelete
  3. Kwa maelezo zaidi kuhusu banki zinazofuata sheria za kiislam soma
    http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

    ReplyDelete

  4. Anon wa pili.

    There is NO way you can avoid mixing religion with business, you are so naive.

    In Islam, religion is a WAY OF LIFE...Business and Politics INCLUDED.

    In Christianity, Vatican, amongst many other things, BANKING is included. BANKING. A very successful and powerful Banking system indeed.

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa Pili Anonymous wa Mon Nov 05, 04:40:00 PM 2012

    Usichukulie moja kwa moja ya kuwa bila RIBA huwezi kukuza yaani,,,''don't think that you cannot attract growth or profit without interest!''

    BASIS /DEFINITION OF INTEREST:
    It is determined by (i)Money supply (ii) Liquidity preference, kitu ambacho sio kweli na UCHUMI WA KIFEDHA WA KIISLAM UNAEGEMEA ZAIDI KWENYE MUAMALA WA MAKUBALIANO YAANI 'COMPLIANCE' NA SIO INTEREST HUKU VITU VINGINE VIKIWA WAZI WAZI TOFAUTI NA INTEREST BASED IKIWA INAFICHA KUANZIA SUALA LA INATUMIA KIGEZO KUTAMBUA YA KUWA RIBA NI % FULANI?

    NDUGU YETU SASA JIBU LA HIYO SINTOFAHAMU LINALETWA NA MISINGI YA UCHUMI NA KIFEDHA YA KIISLAMU MABAYO INAKUWA NI WAZI NA SAWA KWA SAWA KWA NJIA YA MARIDHIANO AU MAKUBALINAO YAANI 'COMPLIANCE'.

    Ndio maana pana tofauti ktk meza za Meneja wa Fedha baina ya Mifumo miwili ya Kifedha:

    1.MFUMO WA RIBA:
    Juu ya Meza ya Menaja wa fedha utakuta pana Kalenda ili kutanmbua ni lini Mkopajia atamaliza deni, na Kikokotozi (Calculator) ili kutambua ni riba Kiasi gani Mkopaji atalipa, huku kukiwa na kitabu cha kuandika Dhamana ya Deni au Mkopo kuwa ni mali isiyoondosheka itakayoshikiliwa na Mkopeshaji hadi Mkopaki alipe.

    2.MFUMO USIO WA RIBA:(ISLAMIC)
    Utakuta Hati za Mikataba ya makubaliano ya Ukopaji, Kikokotozi (Calculator) ipo isipokuwa sio kwa kutoza Riba ila kwa kupiga mahesabu ya gawio la Faida kati ya Mkopaji na Mkopeshaji
    -----------------------------------
    KWA HIVYO GROWHT AU UKUZAJI UPO KTK MISINGI ISIYO YA RIBA 'ISLAMIC' KWA KUWA KIWANGO CHA RIBA (RATE OF INTEREST) DAIMA KIPO CHINI YA GAWIO LA FAIDA KTK MSINGI WA KIFEDHA WA KIISLAMU!!!

    KWA NINI?, MARA NYINGI MAGAWANO KATI YA MKOPAJI HAYATOFAUTIANI SANA HAIWEZI KUSHUKA CHINI YA 40% KWA 60% ZAIDI YA 50% KWA 50% HUKU IKITAMBILIKA YA KUWA DUNIA NZIMA HAKUNA BENKI YA RIBA ITAKAYOTOA ZAIDI YA 30% LAZIMA IWE CHINI YA HAPO !!!

    ReplyDelete
  6. I,for one,I hate mixing Religion with Business or Politics!Biashara misingi yake ni ile ile,iwe nchi za Kibepari au za Kijamaa au Kikomunisti au za Ki-Liberali!The Profit-Motive is the drive,nothing else,asikudanganye mtu Kaka!Ukibisha,hebu endesha biashara yako kwa hasara,uniambie!eti unatoa msaada,au wewe mtu mkarimu sana,biashara haina urafiki na mtu!Ukichanganya Dini na Siasa ndiyo kabisa,sawa,na kuzima moto kwa mafuta ya petroli!wenyewe mnajionea machafuko yasiyo kwisha sehemu mbalimbali duniani!Tuache kudanganyana jamani!Business shall always be for profit!How much profit?hapo ndio watu wanapo tofautiana!ushanfahamu!

    Ni kutokana na fikra kama hizi ndio maana baadhi ya dini zikaacha mafundisho ya mungu na kufuata ya wanadamu kama vile kula riba, kunywa pombe, uzinzi kabla ya ndoa n.k Hatupaswi kupindi sheria za Mungu ili ziendane na"motives" zetu bali tuzipinde motives zetu ziendane na sheria za Mungu.
    Ushanifaham sana!?

    ReplyDelete
  7. Kwa ndugu ambae alishindwa kufahamu tofauti iliyopo kati ya biashara ianyofuata misingi ya kiislam na akadai kwamba biashara zote misingi yake ni ileile kuna kitu ambacho inaonekana hajakifahamu. Biashara misingi yake ni tofauti na kuna tofauti kubwa kati ya biashara inayofuata misingi ya kiislam na zile zisizofuata misingi hiyo. Kwa mfano, biashara za kawaida ambazo umezitaja hua hazijali biashara unayoifanya nihalali au haramu, kama vile biashara za ngono, mkopeshaji tuu ndie anayelindwa na biashara hiyo kwa maana kama ikipatikana hasara ya aina yoyote basi mjasirimali ambae amekopa anapoteza kila kitu hata kama hakuna uzembe wowote alioufanya, kuna kubahatisha kwa hali ya juu ktk makadirio ya faida ‘Excessive risk’ ambayo inachanganyika na hadaa, kamari na kuwafanya watu wengi kupoteza mitaji yao, mitaji mingi ya watu inakua ni mahesabu tu bila rasilimali za kutosha ambazo kama biashara ikipata hasara rasilimali hizo zinaweza kutumika kama rehani ya kufidia hasara iliyopatikana, kinachoangaliwa ni faida tu na hakuna kujali ubinadamu wala jamii, kwa mfano kama umekopeshwa pesa ukaweka dhamana nyumba, baadae ukapoteza kazi, basi nyumba yako itauzwa tu bila kujali ubinadamu na mengine mingi. Kinachotofautisha biashara zinazofuta sharia za kiislam ni kuangalia sana upande wa kibinadamu kuliko faida, kujiepusha na biashara za haramu ambazo zinamdhuru binadamu, kumlinda mkopeshaji na mkopeshwaji kwa mfano kama ikitokea hasara kati ya washirika wawili basi alietoa mtaji atapoteza mtaji wake na mhangaikaji atapoteza juhudi zake, kugawana faida na hasara kwa kiasi cha faida itakavyo patikana na sio kwa kuahidiwa kua utapata faida asilimia fulani bila kujua faida kiasi itapatikana kitu ambacho humsababishia mmoja wa washirika hasara au kupunjwa, kuangalia maslahi ya jamii kama jamii na sio maslahi ya mtu mmoja kujilimbikizia mali nyingi wakati jamii inateketea na mengine mengi. Hizo ni baadhi tu ya tofauti lakin ukitaka kujua zaidi chukua wakati kidogo ili uusome na uufahamu vizuri uchumi naofuata sharia za kiislam.

    ReplyDelete
  8. NIMEFURAHI HUYO MDAU HAPO JUU KUELEZA HISIA ZAKE ZA KUCHUKIA KILE ALICHOKIITA KUCHANGANYA DINI NA BIASHARA.
    ITAKUWA NI KOSA KUBWA AKIACHWA ASIPEWE ELIMU KIDOGO KUHUSU MSIMAMO WA UISLAMU JUU YA DUNIA NA NYANJA ZAKE ZA MAISHA.
    KWA TAARIFA YAKO MDAU NI KWAMBA UISLAMU NI MFUMO KAMILI WA MAISHA AMBAO UNAJUMUISHA KILA KIPENGELE CHA MAISHA KAMA VILE UCHUMI, AJIRA, CHAKULA, SIASA, ELIMU, NA HATA USTAWI WA JAMII. UISLAMU UNA MIONGOZO KAMILI JUU YA KILA KIPENGELE CHA MAISHA KUANZIA KUZALIWA HADI KUFA. KUANZIA KUAMKA HADI KULALA. NI MFUMO KAMA ULIVYO UBEPARI AU UKABAILA. MIFUMO YA KIBINADAMU HUWA NA MWANZO NA MWISHO LAKINI SI MFUMO WA UISLAMU AMBAO MWANZILISHI NA KIONGOZI WAKE NI MUUMBAJI WA KILA KITU.
    KWETU WAISLAMU TUNAELEWA KUWA MFUMO WOWOTE WA KIBIASHARA ULIOBUNIWA NA BINADAMU UNA KASORO NYINGI TU LAKINI SI MFUMO WA ALLAH AMBAO NDIO UNAOFATWA NA UISLAMU. HIVYO NDIVYO TUNAVYOAMINI KWA USHAHIDI WA KUTOSHA.
    KAMA KUNA DINI AMBAYO MIFUMO YAKE YA KIBIASHARA NI YA KISADAKA SADAKA, UISLAMU HAUKO HIVYO. WALA USIDHANI BIASHARA YA KIISLAMU NI YA HASARA HASARA, LA HASHA. NAKUTAMANIA MDAU UACHE UVIVU NA UUSOME UISLAMU UTAELEWA NAZUNGUMZA NINI.
    ULIMWENGU UMEJAA UPUUZI, NA MOJAWAPO YA UPUUZI NI KUDHARAU BADALA YA KUELEWA. MDAU NAKUSHAURI KWANZA UELEWE KISHA NDIPO UFIKIRIE KAMA UNA NAFASI YA KUDHARAU AMA VINGINEVYO.
    KAMA KUNA DINI AMBAYO MFUMO WAKE WA KIBIASHARA NI WA KUPOTEZA MALI, UISLAMU HAUKO HIVYO MDAU. WADAU TUFANYE KWANZA UTAFITI NDIPO TUAMUE KUFIKIRI, KWANI KUFIKIRI BILA ELIMU NI KICHEKESHO.
    SASA NA TUJIULIZE, MBONA BASI HIZI BENKI NA MASHIRIKA YA KIISLAMU YANAYOENDESHA BIASHARA KWA MTINDO WA SADAKA, KAMA KWELI, HAZIFILISIKI?
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  9. I dont care kama ni uchumi wa kufuata misingi ya imani gano. Nachojali ni kwamba nikienda mbali hata kama mimi ni (nachukia jina hili) kafiri, napata huduma so nitaboresha maisha yangu na ya wanaonitegemea. Hilo tu! Ila zikianza za lazima niwe Ally au Ahmed.... Itakuwa si kitu kizuri

    ReplyDelete
  10. Imani na biashara? we are talking about real things in business and not unjustified beliefs and fairy tales from our primitive past. ati allah/mungu ndio muumbaji, how's that going to help my business make money? you will be in business as long as you have something that the market needs and market it well. hayo mambo ya allah na vingine ni sideshows tu and have no real place in business. grow up folks and think for yourself for once and not take things from your "holy" books. what we need is regulations if greed gets out of control and not allah/any other god!
    na kwa kumjibu mdau wa "IJUE BANK YA KIISLAM" Ni bank gani inakupa mkopo bila collateral au at least a sound business plan? kwa nini uingize imani ndani ya biashara? lengo la dini ni ku control maisha ya watu kwa kuwatia woga na vitisho vya kiama na judgement. kama unaamini ni imani yako, lakini there's no truth bearing whatsoever!

    ReplyDelete
  11. Richness in diversity. Wa ku Bank na Vatica waende, Islamic waende, Equity waende; Covenant Bank waendeeeee! Soko huru! Huko huendi kumtafuta Mungu au?

    Kinachotunyima maendelea siyo Bank; Ni TABIA ZETU (our attitudes towards work).

    ReplyDelete

  12. Hapa tatizo la huyu mdau wa PILI ni upeo mdogo hata kwenye mfumo wa hiyo Imani yake.

    Kama mtu aliyekurupuka kutoka usingizini. Na ndiyo walio wengi, wameshibishwa dhana potofu.

    ReplyDelete
  13. Anonymous no 9 sio lazima uwe muislamu ili kupata huduma za benki zinazofuata sheria za kiislam na hapa ndipo wengi wananpochanganya. Umeonyesha kwamba hujali misingi ya imani gani unafuata, hilo linatuchukua kwenye hatua nyingine kwamba inawezekana huna imani yoyote lakin wacha ufahamishwe kwamba ili kupata huduma hizo sio lazima pia uwe na imani kabisa! Umezungumzia kuboresha maisha yako na yawanaokutegemea labda ufahamishwe kwamba hayo hayapatikani ktk misingi ya uchumi mibovu kama baadhi ya ndugu walivyozielezea athari za uchumi mbaya hapo juu. Ni kutokana na misingi hiyo ndio tunahimizana kwamba hakuna faida ya uchumi ambao hautilii maanani ubinadamu. Kama uchumi utaendesha ktk mazingira sahihi basi wewe na wanaokutegemea mtapata huduma na mtaboresha maisha yenu na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  14. Ukweli umeisha simama na uwongo umeisha jitenga. Ama kwa uhakika mwenyezi mungu ni mwenye kutimiza miahadi yake. Tutazunguuka,tutakataa lakini mwisho wetu tutarejea kwake tu tupende tusipende. Hatutaweza kamwe kuizima nuru yake kwa vinywa vyetu.Mwenyezi mungu turuzuju ilm na ufaham.

    ReplyDelete


  15. Mdau wa NOV 6, 09:56:00 AM

    BIASHARA NA SIASA NI SEHEMU YA IMANI, HUWEZI KUVITENGANISHA.

    SIYO MADA HAPA, MADA YA HAPA NI MASUALA YA BENKI, PITIA KWA KITUO MICHANGO YOTE UTAPATA PICHA.

    HAPA HAPAZUNGUMZIWI MASUALA YA IMANI, PANAZUNGUMZIWA MASUALA YA BENKI.

    NI TECHNICAL ISSUES, ADVANCED BANKING KNOWLEDGE. FUATILIA/ISOME ISLAMIC BANKING SYSTEM, NA GENERAL BASIC BANKING UTAELEWA. AU TAFUTA MTU AKUFAHAMISHE.

    MAANA UNALETA MADA TOFAUTI, CHUNGUZA, JIBU LA SWALI ULILOMUULIZA "IJUE BENKI YA KIISLAMU" UTALIPATA.

    NI SUALA LA KUELEWA, HUU SIYO MJADALA. UNAPEWA TAARIFA. KAMA HUJAELEWA ULIZA UTAFAHAMISHWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...