Habari na Picha Na John Nditi, Morogoro 
 WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto, Sophia Simba amesema , tatizo la ukosefu wa ajira si jambo la kupuuzwa ,kutokana na vijana wengi wanaingia katika soko la ajira bila kuwa na stadi kutoka mfumo wa elimu nchini hususani vyo vya ufundi. Simba alisema hayo  katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi katika Vyuo vya Mendeleo ya Wananchi nchini iliyofanyika katika Chuo cha Ualimu na Ufundi Stadi Morogoro ( MVTTC). 

Mhe Simba alisema , tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa kwa kuwa takwimu zinaonesha mwaka 2011/ 2012 vijana 758,371 huingia katika soko la ajira bila ya ujuzi wowote , kati yao vijana 459,931 sawa na asilimia 47 wahitimu wa elimu ya msingi hawakuendelea na masomo ya sekondari.  Wahitimu 298,440 sawa na asilimia 88 waliohitimu kidato cha nne hawakuendelea na kidato cha tano na hawakupangiwa mafunzo yoyoe , jambo linalodhihisha vijana hawana uwezo wa kujiajiri wala kuajiriwa kwa vile hawana stadi zozote za kukabiliana na ushindani katika soko la ajira. 

 Hivyo amesema Ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira , vyuo vya 25 vya Maendeleo ya Wanananchi vitaanza kutoa mafunzo ufundi stadi baada ya Wizara hiyo kwa kushirikiana na Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi Morogoro kwa maadalizi yatakayowezesha washiriki kupata mafunzo ya msingi katika kutekeleza majukumu mapya kwa ufanisi na tija. 

 Katika kufikia hatua hiyo, Waziri Simba ameipongeza VETA kwa kuendelea kubuni na kutoa stadi mbalimbali ambazo huwawezesha vijana kushindana katika soko la jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba dhamira ya Serikali ya awamu ya nne ni kuhakikisha kuona kasi ya kuongeza idadi ya wanaonufaika na stadi hizo inaongezeka. 

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, Kijakazi Mtengwa alisema , vyuo 25 kati ya 55 vya Maendeleo ya Wananchi vitatoa mafunzo ya ufundi stadi ambapo kila chuo kitaanza kwa kusajili kwa wanafunzi 50 kuanzia Januari 2013. 

 Alisema hivi sasa Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA), imeanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi na wakufunzi 100 wa Vyuo hivyo katika awamu mbili itakayofikia tamati Desemba 6, mwaka huu. 

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mafunzo baada ya kuhitimu watasimamia mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyoteuliwa kufundisha mafunzo ya stadi za ufundi kwa vijana wanaohitimu elimu ya msingi na sekondari ambapo wengi wao wanaishi vijijini.
 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ya Watoto, Sophia Simba akikata utepe  kuashiria uzinduzi wa vitabu vya mitaala na vitendea kazi vya mafunzo ya ufundi stadi kwa wakufunzi na wasaidizi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi , vilivyopo chini ya Wizara hiyo kupitia  mpango wa mafunzo ya ufundishaji mahiri ( CBET) na wakufunzi wa  Chuo cha Ualimu wa Mafunzo ya Ufundi stadi VETA  (MVTTC- Morogoro) ( kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kijakazi Mtengwa na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Veta Stephen Tsoray.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ya Watoto, Sophia Simba akionesha vitabu vya mitaala na vitendea kazi vya mafunzo ya ufundi stadi kwa wakufunzi na wasaidizi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi baada ya kuzindua

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ya Watoto, Sophia Simba katika picha ya pamoja na wadau baada ya  uzinduzi wa vitabu vya mitaala na vitendea kazi vya mafunzo ya ufundi stadi kwa wakufunzi na wasaidizi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...