Pichani Juu na Chini ni Meya wa Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Slaa akikabidhi ng’ombe kwa Naodha wa timu ya Kaza Roho, Rajabu Akili (kushoto) baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya kukuza vipaji yaliyojulikana kama "Diwani Super Eight Cup" ya kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Meya wa Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Slaa akimkabidhi Mbuzi kwa mshindi wa pili Naodha wa timu ya Soko Fc (kushoto) baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya kukuza vipaji katika kata yake yaliyojulikana kama "Diwani Super Eight Cup" jijini Dar es Salaam.
Meya wa Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Slaa akimkabidhi Jezi kwa mshindi wa tatu, Zacharia Jonas Naodha wa timu ya Ball Kipaji (kushoto) baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya kukuza vipaji yaliyojulikana kama "Diwani super Eight Cup" ya Kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...