Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali(Mst) Fabian Massawe akiuzindua rasmi mnara wa mtandao wa Vodacom katika kisiwa cha Goziba tayari kutoa huduma kwa wakazi wa kisiwa hicho. Kushoto kwake ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo. Vodacom imekuwa mtandao wa kwanza kufikisha huduma za simu za mkononi katika kisiwa hicho cha ziwa Viktoria ikiwa ni utekelezaji wa azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote katika mtandao wa huduma za simu za mkononi na kuwawezesha kubadili maisha yao.
Kutoka Kushoto Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali(Mst) Fabian Massawe, Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Salum Mwalim na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Avera Mosha wakifurahia kuanza rasmi kwa huduma za Vodacom katika kisiwa cha Goziba. Vodacom imekuwa kampuni ya kwanza ya simu za mkononi kufikisha huduma katika kisiwa hicho cha Ziwa Viktoria ikitekeleza azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote katika mtandao wa huduma za simu za mkononi na kuwawezesha kubadili maisha.
Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na wakazi wa kisiwa cha Goziba wakati wa halfa ya uzinduzi wa huduma za Vodacom kisiwani humo ambapo ni mara ya kwanza kwa kisiwa hicho kupata huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Salum aliwahimiza wakazi hao ambao wengi wao wafanyabiashara ya samki kutumia huduma ya M-pesa kujihakikishia usalama wa fedha dhidi ya matukio ya uporaji na uvamizi ziwani na katika ksiwa hicho kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali(Mst) Fabian Massaweakiongea na wakazi wa kisiwa cha Goziba wakati wa halfa ya uzinduzi wa
huduma za Vodacom kisiwani humo ambapo ni mara ya kwanza kwa kisiwa
hicho kupata huduma za mawasiliano ya simu za mkononi.Kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom,Salum Mwalim.
Sehemu ya umati wakazi wa kisiwa cha Goziba wakiitikia salama ya maendeleo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali (mst)Fabian Massawe wakati w ahala ya uzinduzi rasmi wa huduma za Vodacom katika kisiwa hicho. Vodacom imekuwa kampuni ya kwanza kufikisha huduma za mawasiliano ya simu z amkononi katika kisiwa hicho cha Goziba kilichopo katika ziwa Viktoria.
Baadhi ya wakazi wa kisiwa cha Goziba wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe (nyuma mwenye kofia nyekundu) mbele ya mnara wa Vodacom mara baada ya uzinduzi rasmi wa huduma za Vodacom kisiwani hapo ambazo ni huduma za kwanza za mawasiliano ya simu za mkononi katika historia ya kisiwa hicho kilichopo katika ziwa Vikroria, wilaya ya Muleba.Kushoto kwa RC Massawe ni Meneja Mahusino ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo na Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage


.jpg)





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...