Mtaalamu wa mambo ya muziki pichani wa nne kutoka shoto,Matt Nicholson akiwaonesha baadhi ya wadau namna ya ku-apload muziki kwa njia ya kidigital,ili uweze kusikika na kupatikana katika soko la Kimataifa,wakati wa mkutano wa jukwaa la sanaa uliofanyika mapema leo ndani ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Kuhusiana na namna ya elimu ya digitali kwa wasanii wa muziki na mambo mbambali yahusuyo mfumo mzima wa kidigitali kwa msanii,kutoko kwenye mfumo wa analog kuingia kwenye digital.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa,(BASATA),Gonche Materego akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari (hawapo pichani) ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano wa BASATA,katika mkutano wa jukwaa la sanaa kila siku ya jumatatu uliohusu mambo mbalimbali kwa upande wa wasanii kupata elimu ya analog kwenda kwenye mfumo wa digitali na maandalizi yake kwa ujumla.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clods Media Group na mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,wa tatu kutoka kulia,Ruge Mutahaba ambaye alikuwa mmoja wa waongoza mada ya mambo ya elimu ya Analog kwenda Digital kwa Wasanii.Msikilize hapo chini kwa kubofya hicho kitufe.



Mmoja wa washiriki wa Jukwaa la Sanaa,aliyejitambulisha kwa jina la Amani Lukuli akifafanua masuala ya Maudhui kwenye muziki wetu hapa nchini na nje,Amani alijaribu kuhoji kuhusiana na kudumu kwa maudhui ya muziki wa sasa,kwamba kwanini inachukuza muda mfupi kudumu tofauti na muziki wa miaka ya nyuma?! akatolea mfano wa muziki wa kizazi kipya a.k.Bongofleva kwamba unadumu ndani ya miezi mitatu hadi sita,aidha akazidi kuhoji kuhusiana na uvaaji wa wasaniii wetu,vionjo vya muziki wetu ikiwemo na midundo yake,kwamva vyote hivyo tunaiga kutoka Marekani,je tuna juhudi gani za kuhakikisha vyote hivyo kama wasanii wa hapa nchini wanaviepuka na kujijengea heshima utamaduni wao?! 
Mwakilishi wa Kampuni ya Push Mobile,Patricia Michael akifafanua jambo kuhusiana na mikataba mbalimbali ya wasanii katika suala zima la kupata mapato yao kupitia kazi wazifanyazo za kimuziki.
Msanii wa muziki wa nyimbo za asili,Oscar Siboka a.k.a Mfalme Siboka akichangia mada kwenye jukwaa la sanaa,lililofanyika mapema leo BASATA kuhusiana na wasanii kuwa na elimu ya kutoka kwenye mfumo wa Analog na kuingia kwenye Digita,Siboka aliviomba vya habari kusaidia kuutangaza muziki wa kiasili ambao umekuwa ukikosa promosheni kwa muda mrefu.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo Wanahabari na wasanii wakiwa kwenye mkutano wa Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila siku ya jumatatu ndani ya BASATA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...