Uongozi wa Yanga umepanga kuweka kambi ya wachezaji wao nchin Uturuki baada ya sikukuu ya X- Mass.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Abdallah Binkleb alisema timu hiyo itaenda nchini humo kabla ya mwaka mpya kufuatia mapendekezo ya kocha wao Enerst Brandts.

 Alisema timu hiyo ambayo imeanza mazoezi jana kwenye uwanja wa shule ya Sekondari ya Loyala itaweka kambi ya wiki mbili na kucheza michezo kadhaa na timu mbali mbali za nchini humo ili kujiweka sawa tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania bara ikiwa ni pamoja na kombe la Kagame.

"Hii itatoa fursa kwa wachezaji wote kuweza kujumuika pamoja kwani kwa sasa baadhi ya wachezaji wetu wapo wanazitumikia timu zao za taifa kwenye mashindano ya Chalenji nchini Uganda.

"Mara tu mashindano ya Chalenji yatakapomalizika, watarejea nchini kujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao tayari kujiandaa na safari hyo ya Uturuki", alisema akiongezea kuwa awali walipanga kuipeleka timu nchi Afrika Kusini lakini wameamua kupeleka kambini nchini Uturuki kufuatia mapendekezo ya kocha mkuu, kwani kuna 

huduma bora zaidi kwa ajili ya kambi.
"Kocha ana uzoefu na nchi ya Uturuki hivyo alivyotueletea mapendekezo yake ya kupeleka timu, tulimkubalia na kuanza kuandaa maandalizi ya kambi hiyo lengo ikiwa ni kuifanya timu ya Yanga kucheza soka safi la burudani na kupata ushindi.
Binkleb ambaye alimtoa mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage  machozi baada ya kumfanyia umafia wa kumsajili Mbuyu Twite angali Rage akiwa ameshaanza mazungumzo na mchezaji huyo na kumtangulizia kitita cha dola 30,000 alisema Yanga ikiwa Uturuki inatazamiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu mbili 

ambazo watazitangaza hivi karibuni kabla ya safari yao ya kwenda nchini humo.
"Kocha Brandts anaangalia sana Nidhamu ndani na nje ya uwanja, kwani anaamini nidhamu ndio msingi wa timu kufanya vizuri...Pili kocha anapenda kila mchezaji awe na malengo, na si kucheza mpira tu pasipokuwa na malengo, lazma kila mchezaji ajue kabla ya kuwaza kucheza soka nje ya nchi inampasa kupigania kuhakikisha 

anapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu yake.
"Pia wachezaji wakiishi kwa upendo pasipo kuchukiana kutaifanya timu kuendelea kuwa katika hali nzuri na kucheza mpira kwa bidii na kujituma kufikia mafanikio.
Akizungumzia suala la usajili Binkleb alisema kocha wao Brandts ameshawasilisha mapendekezo yake na kwamba kamati yake ya utendaji inayafanyia kazi kwa kuwa muda bado unaruhusu kwani dirisha dogo linafungwa Desemba 15 huku wakiwapandisha wachezaji watatu kutoka timu ya vijana chini ya miaka 20 baada ya Brandts kuridhika na uwezo wao.
Aliwataja wachezaji waliopandishwa kuwa ni mshambuliaji George Banda, kiungo wa pembeni Rehani Kibingu na golikipa Yusuph Abdul. 
Alisema kikosi cha timu yao ya vijana U20  tangu mwezi July kimecheza jumla ya michezo 24 ya kirafiki na mashindano, kikiwa imeshinda michezo 20, imetoka sare michezo mitatu (3) na kufungwa mchezo mmoja  dhidi ya U-20 Ruvu Shooting.
"Kupandishwa kwa wachezaji hawa ni ishara tosha kuwa tumeamua kuijenga timu kuanzia kwa timu ya vijana na kwa sasa ikiwa imefika hatua ya robo fainali ya mashindano ya El Talento Soccer Tournament yanayofanyika katika uwanja Etihad Stadium - Mwananyamala."alisema.
Wakati huo huo Binkleb alitoa tathmini ya mafanikio ya uongozi wao tangu ulipoingia madarakani Julai 15 mwaka huu kwa kudai kuwa Yanga imecheza jumla ya mechi 23 imeshinda  imeshinda michezo 19, sare michezo miwili na imefungwa michezo mitatu ikiwa imefunga jumla ya mabao 52 katika michezo yote ya kirafiki na Ligi na 

imefungwa mabao 14.
Chini ya Mholanzi Ernie Brandts aliyechukua mikoba ya  Tom Saintfiet Tom, ameiwezesha timu hiyo kutoka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu iliyoachwa na Tom na kushika nafasi ya kwanza ikiwa na poinit 29 mpaka sasa baada ya kushinda michezo saba na kutoa sare mchezo mmoja na kufungwa mmoja dhidi ya Kagera Sugar ikifuatiwa na Azam yenye pointi 25.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh..kipindi hiki hilo winter wataliweza hao jamaa zetu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...