Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote
wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya hafla ya kumuaga
Mheshimiwa balozi Ahmada Ngemera (katikati) ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi, hafla hiyo itafanyika mjini Berlin siku ya Jumamosi tarehe 8.12.2012 .
Mhe.Balozi Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania
wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi kwa kuwa
karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania
wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo
Mhe.Balozi Ngemera na msaidizi wake Mhe. Ali Siwa waliutumua kuhamasisha watanzania
waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu
ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya
ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali.
Lakini kazi hiyo ya kuwaunganisha
watanzania, Balozi Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw. Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia
watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda
ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU) Umoja ambao ni chombo
cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia !
UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA HAFLA HII,
TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.
VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.: 59641 BLZ: 71160161
Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera
Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
simu namba +491734297997 au Katibu simu namba 01734744265 .


Nimesikitika sana kusikia kuwa mh balozi
ReplyDeleteanamaliza muda wake hapa Ujerumani, kwa kweli tutammiss sana, amekuwa akituunganisha kwa mambo mengi. Sasa swali je, hizo Euro 20.00 sina shaka kuzilipa, mbona hamjasema sherehe ya kumuaga itakuwa kwenye ukumbi gani?
Au tunatoa tu na ndiyo mwisho wa mambo?