Na Joseph Ngilisho, Arusha.
WADAU mbalimbali wa benki ya NMB mkoani Arusha wameiomba benki hiyo kuanzisha utaratibu wa kuwakopesha wateja wake nyumba za gharama nafuu ili kuwanufaisha na mikopo wanayokopa katika benki hiyo hususani wajasiriamali wenye kipato kidogo.
Pamoja na kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya aina mbalimbali kwa wateja wake , hali hiyo imewawezesha kuwaondoa katika wimbi la umaskini kwa kuanzisha miradi midogomidogo, ila kwa upande wa nyumba imekuwa ni changamoto kubwa kwao kwani bado benki hiyo haijaweza kuwasaidia .
Hayo yalielezwa na wafanyabiashara wananchama wa klabu ya NMB (NMB business club,)mkoani hapa,wakati walipohudhulia mafunzo ya pili ya siku moja ya ujasiriamali yanayotolewa na benki hiyo kupitia virabu vya wajasiriamali vya NMB,ambapo mwaka huu yanayolenga kujua faida na athari za ushindani katika biashara zao yaliyofanyika jijini hapa.
Alisema kuwa, asilimia kubwa ya wadau wa benki hiyo wamekuwa wakichukua mikopo kwa ajili ya kuboresha biashara zao ila wengi wao bado hawajaweza kujenga nyumba nzuri za kuishi hususani wenye vipato vya chini, hivyo endapo benki hiyo itaanzisha mchakato wa kuwajengea na kuwakopesha nyumba za bei nafuu wataweza kuwasaidia kuondokana na changamoto hiyo.
Akifungua mafunzo hayo , Meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini Vicky Bishubo alisema kuwa benki hiyo imeboresha huduma ya mikopo kwa wajasirimali kwa kiwango kikubwa kutoka shilingi milioni 1 na milioni 5 hadi kufikia sh, milioni 10 , hatua ambayo alisema itamsaidia mfanyabiashara mdogo kuongeza biashara zake na kujitanua zaidi.
|
Home
Unlabelled
wateja wa benki ya NMB Arusha wameiomba benki hiyo kuwakopesha Nyumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...