Mwenyekiti wa Muungano wa vikundi vya kuweka na kukopa (UVIMA), Tatu Mgao (kulia), akitoa shukurani kwa WAMA na NHIF kuwawezesha wanachama wa umoja huo kujiunga na masuala ya matibabu ya mfuko huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani, Mkurugenzi wa Operesheni wa NHIF, Eugen Mikongoti  na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wanawake wa WAMA, Tabu Likoko.


 Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananwake wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Tabu Likoko akiwahamasisha wanawake wa Umoja wa Vikundi vya kuweka na Kukopa (UVIMA), wakati wa hafla ya wanachama wa wa umoja huo kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Majohe, Ilala, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti akielezea faida ya kujiunga na mfuko huo, wakati wa kuwaandikisha sehemu ya wanachama 400 wa  Muungano wa vikundi vya kuweka na kukopa (UVIMA),  eneo la Majohe, Ilala, Dar es Salaam. Vikundi hivyo vinafadhiliwa na Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA). Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Uvima, Tatu Mgao na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake wa WAMA, Tabu Likoko.
 Wanachama wa Uvima wakishangilia baada ya kutangaziwa na uongozi wa NHIF , wamekubaliwa kujiunga na mfuko huo ambapo watakaonufaika kwa kulipia ada ya sh. 10,600 kwa mwezi ni watu sita, ambao ni mama, baba na watoto wao wanne.
Baadhi ya wanachama wa Uvima wakiandikishwa kujiunga na mfuko huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hakuna serikali inayo sadia wakinamama mambo sasa ya dini tu. Ukitaka kufanikiwa jiunge na chama cha dini kwenye kanisa, mskitini, temple au organization zinazo endlea kutimia dini kusaidia wakinamama.Kushindwa kudanganya ni viyama winavyo endlea kutimiwa na mifisadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...