Waziri wa maliasili za Utalii Balozi Khamis Kagasheki akihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taifa TBC mara baada ya kutembelea mabanda ya makampuni ya Tanzania yanayoshiriki katika maonyesho ya Utalii ya World Travel Market yanayoandaliwa na kufanyika katika eneo la Excell jijini London nchini Uingereza, yakishirikisha makampuni mbalimbali ya utalii kutoka pande zote za dunia, Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni zaidi ya 55 yakiwa chini ya Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB).
Waziri Balozi Kagasheki amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania katika maonyesho hayo lakini amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze juhudi za kutangaza utalii wa Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya watalii milioni moja kila mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza vitanda zaidi nchini Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea katika mbuga zetu na kufanya utalii kuka zaidi, Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Waziri aliasili na Utalii wa Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais masuala ya Utalii Zanzibar wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM) jijini London leo nchini Uingereza
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea katika banda hilo leo kwenye maonyesho ya utalii ya WTM nchini Uingereza.
Yvone Baldwin Afisa mauzo wa kampuni ya ndege ya Precision Air akimkabidhi zawadi Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe mara baada ya kutembelea banda hilo leo akiongozana na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...