Kaka,
Hivi huko Halmashauri ya Jiji hakuna taratibu za kuhakiki kitu kabla hakijatoka kwenye public.

Hivi ni kweli hawa Watu hawajui Shule hii inavyoitwa? Na hilo Jina la katikati la Rais Mstaafu Mkapa ndio linavyoandikwa hivyo?

Bango hili linalotambulisha kituo cha taksi nimeliona jana nje ya geti la Shule ya Sekondari Ya Benjamin William Mkapa pale barabara ya Uhuru, Dar es salaam.

Kweli bado tuna safari ndefu.

Perez.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Tehe!

    Another Mulugo

    Tehe teh tee!

    ReplyDelete
  2. Kipi Kiswahili sahihi wadau? Gari 10 au magari 10?

    ReplyDelete
  3. Hahahahaa, Mulugo juu juu zaidi! Kanifurahisha alipohojiwa startv anasema hakwenda chuo kikuu direct moja kwa moja...

    ReplyDelete
  4. KWELI SAFARI BADO NDEFU, HAPO KOSA SI IDADI YA GARI/TEKSI ZA KITUO HICHO, ILA NI JINA LA SHULE LILILOANDIKWA NI LA BABA YAKE RAIS MSTAAFU NA PIA LIMEKOSEWA KATIKA HERUFI YA MWISHO NI M NA SIO N (JINA LA BENJAMIN HALIPO). SIKU HIZI KARIBU KILA UNACHOSOMA KINA MAKOSA NDIO KUSEMA HAKUNA WAHAKIKI WA TAARIFA ZINAZOANDIKWA, KILA MTU ANAONA ANAJUA, MAKOSA MENGI NA MENGINE YANAPOTOSHA HABARI. TUWE MAKINI JAMANI, SIO BORA LIENDE HATUTAFIKA.

    ReplyDelete
  5. Acheni majungu nyinyi, mbona kuna madudu mengine makubwa hamtii neno? herufi moja tu keleleee.............

    ReplyDelete
  6. Elimu tu, wengine hawajui kusoma na kuandika na wengine ni kama hao.Benjamin mwingine na William ni mwingine. Bango kubwa kama hilo wangapi wameliona na hawakutambua kosa hilo. Vipofu ni wengi na hakuwa matonya tu.

    ReplyDelete
  7. Shule zote zina majina za viongozi? Hakuna data zina onesha kwamba ukitumia jina la kiongozi basi shule itatoe elimu safi kwa wanafunzi. Mbona shule nyingi zina jina viongozi na hizo shule ndiyo zina matatizo makubwa.

    ReplyDelete
  8. Haijakosewa!

    Bandugu Mwandishi hajakosea kwa kuwa kwa ndugu zetu Wamakonde Mkapa wanaita Nkapa, Mkulima wanaita Nkulima,

    Tena Mwandishi inaonekana amekuja Mjini muda mrefu kwa kuwa katika jina la Mkapa ameandika sahihi badala ya kundika Nkapa.

    Sasa hapo hiyo WiliaM ni sawa tu Kimakonde kuandikwa WilliaN !

    Mpo hapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...