Ankal habari ya kazi,
Aisee naomba niulizie kwa wadau kwa nini miili ya wachezaji wa zamani ilikuwa imekaa kiriadha zaidi na mikubwa kuliko wa siku hizi? Je, tatizo ni nini hasa? Pia msaada tutani ya majina ya hawa walume...
Mdau Pemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Wachwzaji wa zamani ulikuwa unawaona wanamiili mikubwa inawezekana kwasababu wewe ulikuwa mdogo. Hawa wasasa unawaona wana miili midogo kwa sababu wewe umekuwa mkubwa.

    ReplyDelete
  2. kenny mkapa, marehem method mogella,said mwamba. wengine nimewasahau... hiki kikosi ni kama MADRID YA SASA. ...... YANGA DAIMA!!!!!

    ReplyDelete
  3. Wewe #1 umenianzishia weekend yangu vizuri sana.Nimecheka hadi basi.Unachosema kina ukweli kiasi chake,nilipokuwa mdogo kijijini kwetu kuna vimlima nilikuwa naviona virefu siku naviona vifupi.

    Majina kutoka kushoto:Hamisi Gaga(RIP),Said Mwamba(RIP),Simkumbuki,Method Mogella(RIP),Abeid Mziba,Kenny Mkapa,Aliyeinama kama Salumu Kabunda vile.Kwenye BACKGROUND kipa kama Steven Nemes...Weekend njema.

    ReplyDelete
  4. Wewe Anony wa sat Nov, 10, 09:50AM, Steven Nemes hayupo hapa.

    ReplyDelete
  5. Duu aisee mdau umenikumbusha mbali sana. Hiki kikosi nilikipenda sana kuliko vikosi vyote vilivyowahi kuchezea Yanga. Tuwekeeni picha za kikosi kizima tujikumbushe. R.I.P Said, Method na wengine.

    ReplyDelete
  6. Wachezaji wa zamani walikuwa ni wapiganaji na walikuwa na mapenzi na timu haswa.Na walicheza soka la juu na kuishi maisha duni ,hivyo walikuwa wembamba hivyo kuonekana kama wanariadha na wachezaji wa sasa wameweka zaidi maslahi ,kwani soka imebadilika ,hivyo kutokana na maisha mazuri na kipato kikubwa wanakuwa na miili mikubwa na kuonekana ni wafupi.Big up mdau Joe

    ReplyDelete
  7. Gaga(RIP), Kizota(RIP),Mwakalebela, Method(RIP),Mziba,Mkapa na Kabunda

    ReplyDelete
  8. Huyo anayefuata baada ya marehemu Hamisi Gaga 'Gagarino', Saidi Mwamba 'Kizota', nafikiri ni David Mwakalebela akifuatiwa na marehemu Method Mogella, Abeid Mziba, Kenny Mkapa na Salum Kabunda 'Ninja' kwa mbali anaonekana ni Stephen Nemes na panki lake..

    ReplyDelete
  9. Wewe unayesema Steven Nemes hayupo hapa mwombe ANKAL au rudi shule ukajifunze maelezo ya picha.Bora ungesema siyo Steven Nemes.Nimesema kwenye BACKGROUND(sina kiswahili chake kizuri) ya picha,hawa tunawaona hapa wapo kwenye FOREGROUND.Kuna kipa anakuja(au ni refa?) angalia Nyuma ya Kabunda- ana jezi rangi ya bluu/kijani.Ankal somo lako la picha umeacha siku hizi.

    ReplyDelete
  10. Gaga, Kizota,nafikiri huyu ni Aswile, Method, A. Mziba K. Mkapa na Salum Kabunda kama sikosei na mpaka leo Yanga inaiba wachezaji wa Simba ili kupata furaha ya muda mfupi.

    ReplyDelete
  11. Hapo kushoto ni:Hamis Thobias Gaga,Said Nassor mwamba kizota,katikati ni David mwakalebela,Method mogella,Abeid mziba,Keneth pius mkapa,Salum kabunda 'ninja',nyuma kabisa ni Stephen Casmir Nemes...

    ReplyDelete
  12. Huu uzi(jezi) walizovaa ni nzuri sana. Kumbe Yanga sio rangi za njano na kijani tu hata nyeusi, wawe wanachanganya na nyeusi jezi zimewapendeza sana, wakati mwingine si vibaya kuchapisha mfano wa jezi za zamani kama hizi katika picha.

    JohnJohn

    ReplyDelete
  13. Ni kweli wachezaji wa zamani lishe ilikuwa bei nafuu na pia wachezaji walichaguliwa kwa kuzingatia shibe awe mrefu au mfupi.

    Leodgar SHilla Tenga, Mohammed Tall, Mohd Salim, Adam Sabu, Martin Kikwa, Kitwana Manara, Kassim Manara listi ni ndefu.

    Hata Uingereza kuna timu zina sera ya kuchagua wachezaji walioshiba awe mrefu au mfupi Celtic ya Scotland waliwapinya Barcelona ya Messi kwa kuwa na shibe au timu ya England ya Stoke City lazima uwe na shibe na ngangari ili ujiunge nayo.

    Ni vizuri kuchagua wachezaji wenye shibe iwe warefu au wafupi nfano timu za Misri, Cote D'Ivore, Cameroun, Nigeria, Tunisia kwa kutaja chache.

    ReplyDelete
  14. Siku hizi Tanzania hatuko serious na michezo matokeo yake ndiyo hayo mcheza draft anachezea azam na mwendesha baiskeli anakimbia mita 100 olympic!!

    ReplyDelete
  15. hahahahaha kipa alikua ni STEVEN NEMES tunataka kuanzisha ubishi bure! hahahha

    ReplyDelete
  16. Asanteni sana nimekubali NEMES yupo, niliangalia vibaya nimemuona sasa. I liked this squad!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...