Home
Unlabelled
yanga enzi hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Wachwzaji wa zamani ulikuwa unawaona wanamiili mikubwa inawezekana kwasababu wewe ulikuwa mdogo. Hawa wasasa unawaona wana miili midogo kwa sababu wewe umekuwa mkubwa.
ReplyDeletekenny mkapa, marehem method mogella,said mwamba. wengine nimewasahau... hiki kikosi ni kama MADRID YA SASA. ...... YANGA DAIMA!!!!!
ReplyDeleteWewe #1 umenianzishia weekend yangu vizuri sana.Nimecheka hadi basi.Unachosema kina ukweli kiasi chake,nilipokuwa mdogo kijijini kwetu kuna vimlima nilikuwa naviona virefu siku naviona vifupi.
ReplyDeleteMajina kutoka kushoto:Hamisi Gaga(RIP),Said Mwamba(RIP),Simkumbuki,Method Mogella(RIP),Abeid Mziba,Kenny Mkapa,Aliyeinama kama Salumu Kabunda vile.Kwenye BACKGROUND kipa kama Steven Nemes...Weekend njema.
Wewe Anony wa sat Nov, 10, 09:50AM, Steven Nemes hayupo hapa.
ReplyDeleteDuu aisee mdau umenikumbusha mbali sana. Hiki kikosi nilikipenda sana kuliko vikosi vyote vilivyowahi kuchezea Yanga. Tuwekeeni picha za kikosi kizima tujikumbushe. R.I.P Said, Method na wengine.
ReplyDeleteWachezaji wa zamani walikuwa ni wapiganaji na walikuwa na mapenzi na timu haswa.Na walicheza soka la juu na kuishi maisha duni ,hivyo walikuwa wembamba hivyo kuonekana kama wanariadha na wachezaji wa sasa wameweka zaidi maslahi ,kwani soka imebadilika ,hivyo kutokana na maisha mazuri na kipato kikubwa wanakuwa na miili mikubwa na kuonekana ni wafupi.Big up mdau Joe
ReplyDeleteGaga(RIP), Kizota(RIP),Mwakalebela, Method(RIP),Mziba,Mkapa na Kabunda
ReplyDeleteHuyo anayefuata baada ya marehemu Hamisi Gaga 'Gagarino', Saidi Mwamba 'Kizota', nafikiri ni David Mwakalebela akifuatiwa na marehemu Method Mogella, Abeid Mziba, Kenny Mkapa na Salum Kabunda 'Ninja' kwa mbali anaonekana ni Stephen Nemes na panki lake..
ReplyDeleteWewe unayesema Steven Nemes hayupo hapa mwombe ANKAL au rudi shule ukajifunze maelezo ya picha.Bora ungesema siyo Steven Nemes.Nimesema kwenye BACKGROUND(sina kiswahili chake kizuri) ya picha,hawa tunawaona hapa wapo kwenye FOREGROUND.Kuna kipa anakuja(au ni refa?) angalia Nyuma ya Kabunda- ana jezi rangi ya bluu/kijani.Ankal somo lako la picha umeacha siku hizi.
ReplyDeleteGaga, Kizota,nafikiri huyu ni Aswile, Method, A. Mziba K. Mkapa na Salum Kabunda kama sikosei na mpaka leo Yanga inaiba wachezaji wa Simba ili kupata furaha ya muda mfupi.
ReplyDeleteHapo kushoto ni:Hamis Thobias Gaga,Said Nassor mwamba kizota,katikati ni David mwakalebela,Method mogella,Abeid mziba,Keneth pius mkapa,Salum kabunda 'ninja',nyuma kabisa ni Stephen Casmir Nemes...
ReplyDeleteHuu uzi(jezi) walizovaa ni nzuri sana. Kumbe Yanga sio rangi za njano na kijani tu hata nyeusi, wawe wanachanganya na nyeusi jezi zimewapendeza sana, wakati mwingine si vibaya kuchapisha mfano wa jezi za zamani kama hizi katika picha.
ReplyDeleteJohnJohn
Ni kweli wachezaji wa zamani lishe ilikuwa bei nafuu na pia wachezaji walichaguliwa kwa kuzingatia shibe awe mrefu au mfupi.
ReplyDeleteLeodgar SHilla Tenga, Mohammed Tall, Mohd Salim, Adam Sabu, Martin Kikwa, Kitwana Manara, Kassim Manara listi ni ndefu.
Hata Uingereza kuna timu zina sera ya kuchagua wachezaji walioshiba awe mrefu au mfupi Celtic ya Scotland waliwapinya Barcelona ya Messi kwa kuwa na shibe au timu ya England ya Stoke City lazima uwe na shibe na ngangari ili ujiunge nayo.
Ni vizuri kuchagua wachezaji wenye shibe iwe warefu au wafupi nfano timu za Misri, Cote D'Ivore, Cameroun, Nigeria, Tunisia kwa kutaja chache.
Siku hizi Tanzania hatuko serious na michezo matokeo yake ndiyo hayo mcheza draft anachezea azam na mwendesha baiskeli anakimbia mita 100 olympic!!
ReplyDeletehahahahaha kipa alikua ni STEVEN NEMES tunataka kuanzisha ubishi bure! hahahha
ReplyDeleteAsanteni sana nimekubali NEMES yupo, niliangalia vibaya nimemuona sasa. I liked this squad!
ReplyDelete