Wachezaji wa Yanga pamoja na Azam wakiingia Uwanjani.
 Kikosi cha Yanga
 Kikosi cha Azam.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akiipangua ngome ya Azam kabla ya kuachia kiki kali na kuipatia timu yake bao la kwanza.hadi mwisho wa Mchezo Yanga 2-0 Azam.
 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akichuana na beki wa Azam, FC, Said Morad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia
 Golikipa wa Azam, Ally Mwadini akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wao dhidi ya Yanga uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda bao 2-0.Huko Morogoro nako leo Mnyama (timu ya Simba) avutwa sharubu mchana kweupeeee,baada ya kuchezea kichapo cha Bao 2-0 kutoka kwa Wakata Miwa wa Mkoa huo,timu ya Mtibwa Suger.kwa matokeo ya leo,Timu ya Yanga ndio inayoshika usukani wa Ligi kuu kwa kuwa na point 26.
Balozi wa FIFA, Abeid Pele (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa TFF pamoja na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto wakati alipohudhuria mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam FC kwenye uliuofanyika leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pele yupo nchini kwa  ajili ya programu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. TAFSIRI YA JICHO LA TATU (3) KTK MATOKEO HAYA YA MPIRA WA JUMAPILI YA TAREHE 4 NOVEMBA 2012:

    MATOKEO:

    YANGA SC-2
    AZZAM FC-0

    MTIBWA SC-2
    SIMBA SC-0

    MAANA YAKE NI KUWA (YANGA IMEIFUNGA SIMBA KWA MTAZAMO WA JICHO LA TATU)!!!

    YANGA SC-2
    SIMBA SC-0

    NI KUWA MABAO MAWILI YANGA SC ILIYOIFUNGA AZZAM FC DARISALAMA YAMERUKA HADI MOROGORO YAKAZAMA NDANI YA NYAVU ZA SIMBA SC!

    MPO HAPO?

    ReplyDelete
  2. Hatimaye Mnyama ala kisu Morogoro huku akinyweshwa Juisi ya Miwa !!!

    ReplyDelete
  3. Afadhali kelele na ngebe za Msimbazi leo zimesimama ghafla!

    ReplyDelete
  4. Mdau Anonyomus wa Mon Nov 05, 07:24:00 PM 2012

    ,,,ama kweli huo ni zaidi ya mtazamo wa jicho la tatu (30 ni mtazamo kwa mwenye akili za ziada.

    Si mchezo mabao hayo mawili yamezaa Maandamo Msimbazi jana!

    ReplyDelete
  5. Kufungwa kubaya Mwaka Jana ilikuwa Maandamano ya 'Arab Spring' huko Uarabuni.

    Ila jana ilikuwa Mandamano ya Arab Spring yalihamia Msimbazi Klabuni!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...