Afyacheck ni kipindi kipya cha tv ambacho kinakupa fursa ya kujua afya yako. pia utapata nafasi ya kuuliza maswali yakusu afya. na utajibiwa.kipindi hiki kitakua kinaruka kupitia Clouds tv. Hiki hapa ni kipindi cha kwanza cha afyacheck ambapo inazungumziwa swala zima la afya ya uzazi tazama uone mtoto anavyo patikana kila hatua inaonekana mpaka mbegu zinavyo ungana.
Home
Unlabelled
AFYA CHECK - AFYA YA UZAZI (REPRODUCTIVE HEALTH) ON CLOUDS TV
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
afya check kweli bongo tambarare. Kwahiyo watu wamekaa kabisa na kukubaliana hilo ndo jina la kubeba kipindi? afya check!!
ReplyDeleteSasa mdau hapo juu wewe ungependa kiitweje? Au unapinga tu?
ReplyDeletewatu mnapinga pinga kila kitu!!! badala ya kupongeza uzuri wa kipingi mnaanza kubishia jina lake!!! kweli binadamu hatosheki...madokta kazi nzuri
ReplyDeletekama ni kiswahili basi kitumike kiswahili na kama wanataka kingereza waitumie hiyo lugha. Sasa kweli kipindi kinabeba kiswanglish?
ReplyDeleteWadau kuna kitu kimoja naomba kutofautiana na wasomi wenzangu tunaozungumza lugha ya Kiswahili. Nakubali kuwa kuna kipindi inabidi tutumie lugha ya Kingereza maana ndiyo inayotumika katika kutoa elimu. Tatizo ni pale tunaposema "..kwa kitaalamu inaitwa embryo..",..wataalamu wanaita DNA.." Hilo limekuwa likinikera kwa muda mrefu kuona msomi anaongea neno la Kiswahili halafu tafsiri yake kwa Kingereza inakuwa kwa lugha ya kitaamu. Kwa hiyo wote wasiozungumza Kingereza siyo wataalamu? Mimi nilifikiri hawa madaktari ni wataalamu, lakini wao wenyewe wanakana kuwa siyo, hadi pale wapotumia Kingereza (kitaalamu). Ukoloni uliisha miaka 51 iliyopita. Kama tumeamua kujidharau sisi waswahili, basi si vema kudharau mataifa mengine yasiyotumia lugha ya kitaalamu a.k.a Kingereza.
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu, jina hilo la kipindi halina tatizo lolote.
ReplyDeletekwa keli kipindi ni kizuri kina elimu kibao.big up clouds.
ReplyDeletesasa basi naomba kujua hiki kipindi kinarushwa lini na saa ngapi?ni vyema Dr. Isaack naomba unapotambulisha kipindi eleza pia siku na wakati kinaporushwa kwenye tv.
kila la kheri kwa mwaka 2013.
Susan