Balozi Celestine Mushy (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Bibi Joyce Mends-Cole, Mwakilishi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hapa nchini. Bibi Mends-Cole alifika Wizarani kwa madhumuni ya kujitambulisha.
Bibi Mends-Cole akizungumza na Balozi Mushy alipofika kujitambulisha.

Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza na Mhe.  Debnath Shaw, Balozi wa India hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na India.
Balozi Kairuki (kulia) akipokea barua ya mwaliko kutoka Balozi Debnath   kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamataifa wa kuhudhuria Maadhimisho ya Taifa la India yatakayofanyika  mwezi Januari, 2013.

Balozi Kairuki akiendelea na mazungumzo na Balozi Shaw. Wengine katika picha ni Bi. Redemptor Tibaigana, Afisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Asia na Australasia na Bw. Gopal Krisha Pant (wa kwanza kushoto), Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini. Picha na Rosemary Malale

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...