Kaka Michuzi ajali hii mbaya imetokea lao Tarehe 31/12/2012 mida ya saa 10:20 jioni maeneo ya TOANGOMA.
.
Ajali ilihusisha gari aina ya Toyota Surf pamoja na Min-Canter ambapo zote zilikuwa zinatokea barabara inayounganisha Kongowe na Kigamboni..
.
Mwenye Toyota Surf ni mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi na inasemekana alikuwa amesimama akiwa amewasha indiketa ya kuingia kulia kuelekea nyumbani kwako ambapo nyuma yake tayari kulikuwa na magari matatu yakiwa yamesimama yakimruhusu na kumsubiri aingie kwake..
.
Baada ya kuona ameruhusiwa kwenye "Site Morror" ndipo alichukua uamuzi wa kuingia mara ndipo ilitokea Kenta hiyo iliyokuwa imebeba Kokoto ikiwa kwenye kasi ya ajabu na kuibamiza Toyota Surf hiyo kwenye mlango wa nyuma na hatimaye kuiburuza hadi kwenye mtaro kama inavyoonekana..
.
Mwanajeshi huyo aliyejulikana kwa jina moja tu ka Bw. KAMUNDE alikuwa na mkewe ndani ya Surf hiyo lakini kwa maajabu ya Mungu woote ji wazima wa afya na walikuwepo salama salmini kwenye eneo la tukio wakiwaeleza wananchi na askari polisi wa usalama barabarani namna ajali ilivyotokea..
.
Hata hivyo dereve wa Kenta hiyo aliingia mitini baada ya tukio hilo. Kunusurika kwa wote katika tukio hili ni mapenzi ya Mungu tu maana hali ya magari yote haitamaniki. .
.
Jamani tunawaimba Madereve wote na kuwasihi kuwa waangalifu hasa kipindi hichi cha mwisho wa mwaka. Jeshi la polisi ni vyema likajipanga vya kutosha kukabiliana na udereva zembe ambao unaweza kugharimu maisha ya watu pasi na sababu kama ilivyotaka kutokea katika tukio hili..
.
Habari na mdau Herman Edgar Berege, TOANGOMA.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haya kikowapi? hata kokoto za watu hujafikisha, umeziacha na ukaamua kukimbia. Mimi kila siku huwa najiuliza, kama haya si makusudi kwanini maana kila inapotokea ajari mbaya iwe imehusisha vifo au uharibifu yule ambaye mwenye makosa siku zote huwa anawahi kukimbia kila taarifa ninayosoma ni hivyo, kwahiyo ni kwamba huwa wanafanya makusudi na dawa yao iwapo wanapatikana basi kuwapa adhabu kali ikiwemo kuwaonesha moja kwa moja kupitia Tv labda itasaidia.

    ReplyDelete
  2. Poleni wote mlionusurika, ila naomba kutoa angalizo, sehemu hiyo inaitwa TUANGOMA sio Toangoma

    ReplyDelete
  3. Pole sana hizi ajali hizi .... tuombe mwaka huu mpya tuwe makini barabarani .... Ankal sijaelewa hapo kwamba magari matatu yapo nyuma yake yakamruhusu aingie .... au mimi ndio sielewi

    ReplyDelete
  4. Kama serikali haitakuwa waangalifu kuhusu tatizo la usalama barabarani basi kwenye sensa ijayo tutakuwa na upungufu wa watu. Naomba kutoa ushauri kwa serikali kuwa kuwa na zero tollorance attitude kuhusu usalama barabarani kwa mfano:
    -Faini na vifungo.
    -Kupingwa marufuku madereva wazembe.
    -Ku-improve road signs.
    -Dereva asiendeshe mpaka awe amerudia theory test kila baada ya miaka 5.
    -Kuongeza askari wa barabarani.

    ReplyDelete
  5. Wekeni matuta jamani hawa madereva vichaa wanatumaliza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...