Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar wakiisubiri timu ya wazee kwa ajili ya mechi iliyoandaliwa na chama cha mpira huo huko katika uwanja wa Mau.
 Mwandishi wa habari kutoka Chuchu FM Redio Yahya Saleh akimuhoji kocha wa timu ya mpira wa magongo (HOCKEY)  Mgeni Haji  juu ya upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ambapo alisema ni ghali mno.
 Timu ya wachezaji wa zamani wa magongo (HOCKEY) wakiwa katika mapumziko mafupi (Halftime)huko katika uwanja wa Mau.
Mchezaji wa timu ya Kombaini Halifa Abdallah Maabadi mwenye bukta ya njano akisawazisha bao katika mechi hiyo ambayo ilitoka mbili mbli.
 Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar Ramadhan Pandu Makame ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ili waweze kuuendeleza na kushiriki katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Ramadhan ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na chama hicho kwa lengo la kujindaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es laam Januari 09 mwakani.

Amesema Vifaa vya mchezo wa Mpira wa Magongo ni ghali sana kiasi cha wao kushindwa kumudu kuvinunua na hivyo kulazimika kuomba msaada ili wasaidiwe kupatikana kwake.
Ameongeza kuwa Zanzibar kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na ushajihishwaji wa vijana kujiunga na mchezo huo.
Ramadhan amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu chama hicho anaamini kuwa Zanzibar inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindani ya kitaifa na kimataifa.
Akizungumzia kuhusu mashindano ya Mapinduzi Cup Ramadhan amesema mashindano hayo yatazishirikisha timu nane ikiwemo timu ya Zanzibar.

Kwa upande wao Wachezaji wakongwe wa Mpira wa magongo wamekipongeza chama cha mpira huo kwa kuandaa mechi kati yayo na timu ya kombaini ya Zanzibar ikiwa pamoja na kuwashajihisha vijana ili kuupenda mchezo huo.
Aidha wamekishuri Chama hicho kuandaa mechi za mara kwa mara kati yao ili kuipa ukomavu timu hiyo na pia kuutangaza mchezo kwa Wazanzibari
Katika Bonanza hilo Timu ya Maveterani wa mchezo huo ilipimana nguvu na Timu ya Kombaini ya JWTZ na KMKM ambapo matokeo ya mchezo huo ni suluhu ya mabao mawili kwa mawili.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hockey Zanzibar haina wachezaji wepya. Hao wenyekucheza nawakumbuka tangu mdogo kuwa ndio hao hao na sasa wameshazeeka. Wengi wao ni majeshi. Ili mchezo huu ukuwe itabidi chama cha mchezo huu watoe uwelewa wa huu mchezo kwa wanafunzi na pia kutafuta vifaa vya kuchezea vya bei ndogo. Mchezo huu ni mzuri lakini ni hatari na matibabu sio rahisi sasa Zanzibar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...