Kikosi cha Zanzibar kilichocheza
Tusker Challenge Cup Uganda

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni miongoni mwa wachezaji 16, waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.
Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.
Hata hivyo katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye jana alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, amesema hatua hiyu ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.
Tayari ZFA Taifa walikwishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa vilabu wanavyochezea wachezaji hao.
Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutatwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.
Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda Challenge ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hiyo inatwa kuchukua sheria mikononi!!

    ReplyDelete
  2. inaonekana viongozi wa ZFA wamekasirika kwasababu marahii wamezulumiwa wao, hahahaha njaa bwana!!

    ReplyDelete

  3. Mh!

    Yaani unamzuia mchezaji kwenda nje kwa kuwa wamegawana dola 10,000??!!!

    Hapo sanasana kila mtu kapata MAXIMUM dola 800!!!

    Sasa dola 800 si mngewaachia tu wafute jasho???
    What is 800$ kwa mchezaji???

    Mnakimbilia ukiwazuia eti kucheza popote duniani!!! Wameua???????
    Ndio maana, kwa mitazamo hii tutazidi kudumaa tu kimichezo, hakuna mtu anayejali vipato vya wachezaji wetu. Hivyo vidola elfu 10,000 wote mlikuwa mmevitolea macho.

    KWANI MLITAKA KUWAPA BEI GANI

    ReplyDelete
  4. Umaskini ni kitu kibaya. Sasa hao viongozi wa ZFA walitaka kuzibania hizo $ 10,000? Umaskini ni kitu kibaya sana!

    ReplyDelete
  5. HAMNA MAHALA POPOTE KATIKA KANUNI ZA ADHABU ZA FIFA ZINAPROVIDE ADHABU KWA KOSA HILO HUO NI UONEZI EBU KAAENI CHINI MUONE JINSI GANI MNAWEZA KULITATUWA JAMBO HILO NA PIA MUJIULIZE KWA NINI WACHEZAJI WAMEAMUA HIVYO KUNA SABABU YA MSINGI NAYO NI KUWA MNAWACHAKACHUWA MARA ZOTE, WACHEZAJI MSIKUBALI FIKENI HATA FIFA KUDAI HAKI ZENU

    ReplyDelete
  6. Hivi hawa viongozi wa ZFF wana akili timamu kweli?Kikosi chenyewe kinajumuisha vipaji vya timu kubwa ,Yanga ,Simba na Azam ,je wanafikiri TFF na Watanzania watakubali?Hatua ichukuliwe ili viongozi wa ZFF wawajibishwe na ikiwezekana ivunjwe kabisa ,kwani haya maamuzi ni ya kibangi sanaaa na si yaliyokwenda shule.Wachezaji wamedai haki yao ,ama kweli ukitaka watu wakuchukie dai haki yako au sema ukweli.Big up ,mdau ughaibuni.

    ReplyDelete
  7. Wafungiwa kucheza popote Amani na ZNZ sio Duniani ZFA ANAITAMBUA NANI?
    Ngoja hizi hela walivunja benki au sanduku wakaiba au walikabidhiwa wenyewe?
    Kama walikabidhiwa ni zao sas wakurudishieni kisha muwape tena hizi ni akili za kitoto-basi hao walorudisha tupeni taarifa kama mmewapa hela kamili.
    Mlitaka mseme tumetumia gharama hizi imebaki dola 200 gawaneni

    ReplyDelete
  8. Hapa hii adhabu ikipelekwa TFF, CECAFA, CAF na hatimaye FIFA itafutwa, ZFA imetumia jazba.

    Wachezaji hawa wanageweza kuzuiliwa kuichezea timu ya taifa la Zanzibar, Zanzibar Heroes iwe ndiyo adhabu yao.

    US$ 10,000 igawanywe ZFA, wachezaji, Baraza la Michezo, TRA sijui wachezaji wangeambulia kiasi gani.
    Mdau
    Mtaa wa Jangwani/Msimbaziholymen 714

    ReplyDelete
  9. kule wengi wao huishi kwa jazba na kutoa maamuzi kwa jazba sasa hiyo ni aibu yao wenyewe kuwasimamisha wachezaji kisa $10000???

    ReplyDelete
  10. ZFA inatambulika wapi!!! Mwizi kaibiwa basi hilo yowe lake!!!!

    ReplyDelete
  11. viongozi wa soka mnatia aibu na njaa zenu yani kuwafungia sababu hizo hela hamjazipata hahahaha

    sasa ukiwafungia ndio nini si uzembe tu maana maendeleo kamwe hayatopatikana

    eti wachezaji wanne ndio walionusurika kutokana na kurejesha hizo hela hahahaha

    njaaa njaa njaa aibu aibu aibu kwa chama cha soka tz.

    ReplyDelete
  12. ZFA haitambuliki rasmi FIFA hence wachezaji wanaocheza nje ya zanzibar adhabu hii haiwagusi kabisa ila pale TFF itakapoamua kukubaliana na ZFA na kuipitisha adhabu hii

    ReplyDelete
  13. sometimes unakaa unafikiri hvi hawa watu waliokwenye hizi ngazi wanakisomo chochote maana hapa sioni reason ya kutoa tamko eti unawafungia wachezaji kutokucheza dunia nzima,ELIMU yako iko vipi wewe mi nafikiri tukuoji,kosa sawa lipo ila ni kuwapa adhabu ya kutokucheza timu ya ZANZIBAR HEROES tu na si vingine acheni akili za panzi nyie watu wa ZFA,na mnajisema kabisa hapa eti mmekaa chini kama kamati kabisa kuwajadili na mwisho mkaja na hili suruhisho,kweli wote nyie mmeshindwa hata kuona mko wrong wote......ELIMU na UPEO wenu wa kufikiri ni duni sana wana ZFA ndo nyinyi hasa mnaozoofisha soka la zanzibar na tanzania kwa ujumla maana mnaonekana hamfikiri kabisa

    ReplyDelete

  14. Anon wa Dec 12, 06:05:00 PM 2012

    HAWA JAMAA NDIO ZAO!!!!!!

    YAANI NI AIBU WALA SIYO YA KUSIMULIA!!!!!
    TUPIGE HESABU, TUSEME JUMLA NI WACHEZAJI KUMI NA TANO (15), ITAKUWA APPROX. WAMEGAWANA $650......SASA?, WHAT IS 650$????

    YAANI WATU NA AKILI ZAO TIMAMU WANAKAA KUJADILI NA KUWATEMESHA WALIOTEMA $650?????

    NAUNGANA NA WADAU WANAOSEMA HAWA NDIO WANAODHOOFISHA SOKA KWA KWELI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...