Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera, akiwa na maofisa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ameongoza opereseheni ya kuwasaka wafugaji walioficha ng’ombe zao kwenye bonde la Kilombero linalojumuisha Wilaya mbili ya Ulanga na Kilombero kwenye maeneo yasiyofikia kirahisi na askari kwa njia ya kutumia miguu ama magari.
Zoezi lililfanyika kwa muda wa siku tatu kuangia Desemba 8 hadi 10 , mwaka huu , ambapo mifugo mingi ilikamatwa na kuondolewa kwenye maficho hayo katika 'Operesheni Okoa Bonde la Kilombero', lililofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Desemba 8 hadi 10, mwaka huu kwenye bonde hilo lililopo pande mbili za Wilaya ya Kilombero na Ulanga kwa kutumia Helikopta ya Jeshi la Polisi.
Mifugo zaidi ya 5,000 iliyokuwa imefichwa maaneo yalisiyofikika ilibainika na kukamatwa kabla ya kupingwa faini na kuamriwa kuondoka ndani ya Bonde hilo na wafugaji hao kutakiwa kurejea na mifungo yao walikotoka kabla ya kufika kwenye Bonde hilo. Habari na picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro.
Mwanzo wa safari |
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwahutubia wananchi wa Kata ya Itete, Tarafa ya Mtimbira, Wilayani Ulanga, alipotua na Helikopta wakati wa kusaka wafugaji waliojificha na ng'ombe wao
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akiangalia uwanda wa sehemu ya Bonde la Kilombero akiwa ndani ya Helikopta ya Polisi |
RC BENDERA AKISILILIZA HOJA ZA WAFUGAJI NA WANANCHI ( HAWAPO PICHANI) KUTOKA TARAFA YA MALINYI, WILAYA YA ULANGA
RC Bendera ( mwenye jaketi ) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kilombero , Maofisa wa Polisi na marubani wa Helikopta ya Jeshi hilo
Sehamu ya mto Kilombero uliopo katika bonde la Kilombero ukionekana toka angani
Sehemu ya Bonde la Kilombero lilivyoharibiwa na mifugo likionekana kutoa agani
Sehemu ya ng'ombe waliokamatwa ndani ya ardhi tengefu ya hifadhi ya Bonde la Kilombero, Desemba 9, mwaka huu eneo la Malinyi, Wilaya ya Ulanga
Ivi ni faida gani inayopatikana kwa hasa wananchi watanzania toka kwa hiyo mifugo ambayo si tu uhalibifu wa mazingira bali imesababisha uhasama karibu ktk kila sehemu ambayo ufugaji utakuwepo?Bei ya nyama haishikiki kwa watu wa kawaida nyama bado yaonekana ni anasa, maziwa pia hayanywiki bei ni juu hivyo bora kununua unga kuliko maziwa sasa najiuliza faida iko wapi? sina uhakika kama tunasafirisha nyama nje ya bara la afrika kutokana na viwango vyetu hivyo basi nini faida ipatikanayo na hawa ngombe?U shamba umetujaa watanzania eti mtu anamiliki ngombe 2000,3000 mpaka 5000 kwa uwiano wa lita moja kwa ngombe watano sasa hapa jamani kuna haja ya kuendelea kufuga kweli?ulaya wenzetu familia inaweza kuwa na ngombe watano tu tena hao ni wengi kweli na bei ya maziwa na nyama ni rahisi kuliko huko nyumbani ambapo mtu mmoja anaweza kua na idadi ya mifugo niliyoitaja hapo juu,Nadhani kuna haja ya serikali kuangalia faida waletazo hawa wafugaji na kulinganisha na hasara waletazo na ikiwezekana kuwatengea kiwango/idadi ya mifugo ambayo wanastaili kumiliki vinginevyo tunakaribisha maafa ya aidha jangwa au mafuriko kwa kuwa na idadi nyingi ya mifugo isiyokua na tija.
ReplyDeleteBila kujali ubinadamu hawa ng'ombe wapigwe mnada kwa ajili ya fundisho kwa wengine!
ReplyDeleteKwa jamii za aina ya ng'ombe inaonekana kwa picha ya chini hawa ni ng'ombe wa aina ya 'Ankole' wakiwa wanatokea kiasili nchini Rwanda.
ReplyDeleteKwa shida ya ardhi ya Jamhuri ya Rwanda ikilinganishwa na msongamano wa watu nchini humo ni mkuwa zaidi kuliko nchi ingine ya EAC (Rwanda-watu 469 kwa Kilometa za mraba, wastani kwa nchi zingine Afrika ya Maahsariki ni watu 50 kwa Kilometa moja ya Mraba) inwezekana wamelitwa na watu wa huko kwa kusaka malisho ikiwa kama sehemu ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na majirani zetu hao!.
Ni kwa nini pasiwekwe uchunguzi kuhusu Uraia wa ng'ombe hao?
Kweli wajameni,
ReplyDeleteHizi pembe ndefu za ng'ombe sio katika aina ya mifugo yetu ya Ki-Tanzania!
Mdau wa 3 wa Wed Dec 12, 12:28:00 PM 2012
ReplyDelete...Ipo kazi kuelekea Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki!
Idara ya Uhamiaji nadhani ni wakati sasa ili kutimiza majukumu muombe Serikalini na Bungeni Hoja ipite ya Pasipoti za mifugo kuanzia ng'ombe!!!
Tulizoea wageni wazamiaji Binaadamu na sasa tunakabiliwa na uzamiaji wa mifugo wageni!
Badala ya Mabanyamulenge kutoka Rwanda na Kongo sasa tunamefikia kufanyiwa uzamiaji na ng'ombe kutoka Rwanda kwa Kagame!
Ama kweli mwanawane ndio maana Bongo Tambarale sio?