Leo hii nimeamua rasmi kurudi CCM, chama ambacho nimekifahamu kwa miaka 35 sasa.
Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha kwenye level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana, Namibia au hata baadhi ya nchi za Ulaya.
Niliamua haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi yatokeayo nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbalimbali.
Nilifanikiwa kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga mikakati ya kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua matawi nchi nzima na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo mmoja. Pia nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.
Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache niliamua kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.
NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA KUJENGWA!
SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.
MAISHA YA WATANZANIA YAMEBADILIKA SANA - MIDDLE CLASS NI MAISHA YA KAWAIDA TU. VIJANA WENGI WAMEENDELEA TOFAUTI NA ZAMANI MPAKA UWE MCHAWI KIDOGO NDIO UWE TAJIRI. MIJI INAJENGEKA KWA KASI YA AJABU. UKIHARIBU KAZINI UTAWAJIBIKA .
Na mengine mengi tu niliyaona mpaka nikaanza kujiuliza , hivi najiita mpinzani, NINAPINGA NINI?
Kama ni maendeleo nayaona tena maendelo original Nikakumbuka msemo mmoja... “KWA NINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO?”
Kwangu mimi CCM ni original na Chadema ni photocopy, tena copy iliyotolewa wakati mashine imekwisha wino. Mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya CCM na si kwingineko!
Kuna mengi mazito yamenichefua Chadema lakini sitayasema leo. Juzi mwenyekiti wangu wa Taifa Mheshimiwa Mbowe alipita hapa UK, lakini, mpaka ameondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema hapa UK kitendo ambacho kiliniuma sana, kwani, niliona kama tumedharauliwa;
BABA HUWEZI KWENDA SEHEMU WALIPO WANAO UKASHINDWA HATA KUWAPIGIA SIMU KUWAJULIA HALI.
Ni matumaini yangu kuwa uamuzi wangu utaeleweka. Kama tujuavyo, kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, lakini naona kwenye msafara wa Chadema idadi ya kenge inazidi mamba.
Chris Lukosi
LUKOSI GLOBAL TRADERS LTD UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RH. OFFICE; 01375 855 915, FAX; 01708 202 477, MOBILE; 0790 3828 119
KWA HIYO UNAKIRI ULIFUATA MKUMBO SASA JITAHIDI UWAREJESHE NA WALE WALIDANDIA GARI LAKO,HUTAKIWI KUFIKIRI SANA WAJANJA WOTE WA MJINI HAPA UK WAMEVIMBA NA CHAMA LETU CCM ASAVALI UMESHTUKA MAPEMA WELL COME HOME BRAVE.
ReplyDeleteUlivyojiunga Chadema ulikuwa unaamini kwamba Tanzania haina barabara sio?:)
ReplyDeleteKwani ulikuwa huoni globu ya jamii kila siku inaturushia picha za vikwangua anaga?:)
Pole kaka. I thought u were smarter than that.
(US Blogger)
Huyu jamaa vp?yaani wewe kuishi kote huko ulaya haya mabadiliko na mafanikio uliyoyataja mbona yanaoneshwa ktk hizihizi blogs ambazo sisi pia tulio mbali na nyumbani hua tunayaona na kusoma? mengi nimeyagundua baada ya kusoma hii taarifa,binafsi si mshabiki wa chama chochote japo naguswa kama mwananchi na mengi yanayotokea nyumbani,mchango wa vyama pinzani vya siasa ni mkubwa sana pengine hata zaidi ya uelewa wa huyu bwana ktk hayo mafanikio yoote uliyoyataja.kwa ufahamu na uelewa huu wa huyu bwana sidhani kama kuna haja ya kutiliashaka maamuzi yaliyofikiwa juu ya kumtimua huyu bwana.Maelezo yote aliyoyatoa yana akisi ufahamu mdogo sana alionao huyu bwana nahisi alipewa madaraka makubwa kuliko uelewa wake nadiriki wakati mwengine tunafanya makosa kwa kuangalia vigezo vingine visivyo sahihi ktk kumkabidhi mtu jukumu zito kama alilopewa, kwa kuthibitisha haya niliyoyasema ebu jaribu kuangalia ni muda gani umepita na haya maamuzi aliyoyachukua nahisi kama amekurupuka bila ya kujipa muda na kutafakari.
ReplyDeleteHongera sana kaka yangu. Ujumbe umekaa safi kabisa nanimekuelewa.
ReplyDeleteUsemakweli ilinishangaza sana kuona watu wanaandika ujumbe ati haa Chris hayuko chadema tena. Mtu kaandika kwa hasira, bila mpangilio wowote. Ujumbe wako umekaa vizuri.
Najua kuwa wewe ni mtu wa kuaminika kabisa na umesaidia watu wengi.
Ila sasa hivi achana na kusoma comments ambazo nadhani kuna wendawazimu wataziweka na mimi nadhani watakuwa wachafua hewa tu.
ni hayo tu
Kinyenyefule Nungunungu.
Hii ni izitaki mbichi hizo!!
ReplyDeletenjaa mbaya
ReplyDeletewewe usichafue chadema kwakuwa ulichokuwa unatarajia hakikufanikiwa.mimi kwanza bila shaka ulishakana uraia wa Tanzania, nashangaaa unacholalamikia ni nini?tuachie nchii yetu sisi tunaoishi ndo tunajua tunataka mabadiliko gani?hivi wewe unaona mabadiliko ni chuo na sekondari za kata ambazo hazifahulishi.kwa miaka hamsini sasa TANZANIA ingetakiwa iwe mbali kuliko kenya kwa rasilimani tulizonazo lakini badala yake Viongozi wetu wanaficha pesa ulaya,hiyo ni akili matope, sawa basi laiti wangewekeza nchini watu wakapata hajira watu wanamaliza chuo hawana hajira.tunatia aibu yani mwananchi wa kawaida anaishi kwa mloo mmoja wengine wanawasha vijinga wapate kuona wanako lala hawana shs mia tano ya mafuta ya taaa.NDUGU YANGU NAOMBA KAMA WEWE ULITAKA MWENYEKITI LAZIMA AKIJA AJE AKUPIGIE MAGOTI BADALA YA KUTIMIZA WAJIBU WAKO KAMA KWELI ULIKUWA NA NIA YA MABSDILIKO NAKUPA POLE HATA UKO ULIKO JIUNGA UTAKUWA HIVYO HIVYO MAANA HUIAMINI ALIMASHAURI YAKO YA KICHWA.NA HUFAI KATIKA JAMIII.
ReplyDeleteKumbe ulikuwa hujui nyumbani kwenu kwa miaka yote hiyo. Wewe huna ndugu? Sidhani kama CCM utatusaidia,ungefanya biashara tu
ReplyDeleteAcha longolongo kama umeona mambo yamekushinda toka kimyakimya,mbona ulipoingia chadema hukututangazia kwanini ulingia?! Halafu ndugu yangu kuwa na barabara nzuri ni wajibu wa serikali siyo maendeleo shule, hospital nzuri ni wajibu wa serikali yoyote duniani,ji sawa na unapomzaa mtoto jukumu la kumlea kumtunza ni lako wewe baba ,huwezi kusema mwanao umemfanyia fadhira sasa ulitaka alelewe na nani?!!
ReplyDeleteWEWE NI NYOKA NA NDUMILA KUWILI HATA HUKO CCM UTATOKA MAANA SIDHANI SABABU ZA KUJENGWA KWA BARA BARA NYINGI BONGO HUKUWA UNAJUWA NA UMEJUWA SIKU CHACHE BADA YA CHADEMA KUYUMBA UK
ReplyDeleteWEWE NI MUONGO MAANA KAMA KWELI UMEWEZA KUTOA TAARIFA YA KUJIUZULU KWENYE BLOG YA ISSA MICHUZI BASI WEWE UMEKUWA UNAFAHAMU UZINDUZI WA BARA BARA ZINAZOJENGWA BONGO
SIYO POINT HATA KIDOGO. JE NA UFISADI NA RUSWA AMBAZO ZDIO ZIMETAWALA CCM NAZO UNASEMAJE?
WEWE UNGEKUWA MUUNGWANA USINGEJITANGAZA KUHAMIA CCM NA KUIPONDA CHADEMA. KAMA SIYO CHADEMA ILIYOLETA USHINDANI BUNGENI NCHI HII INGEKUWA KATIKA HALI MBAYA ZAIDI
WAPINZANI WAMESAIDIA SANA BONGO
NEDA KWA SALAMA CCM ACHA KUPONDA CHADEMA WAKATI ULIKUWA NA AKILI TIMAMU KUINGIA HUKO MPAKA UKAWA MWENYEKITI
SUBIRI NAO WATAKUPA CHEO SASA HIVI
hapa naona kuna jambo mojawapo au yote mawili kwa pamoja,yaani njaa au/na uelewa mdogo.
ReplyDeleteje alikuwa blogs na vyombo vingine vilikuwa havionyeshi mafanikio hayo?
Hahah, Kuna kiongozi alishasema Nanukuu "Hukitaka biashara zako zifanikiwe njoo CCM". Naona jamaa kashtuka wataanza kumfuatilia issue za kodi na mambo mengine ya kiusanii.Nipita tu
ReplyDeleteSawa kaka nadhani ni haki yako kujiunga na chama chochote cha siasa,swali langu ni hili ni kweli kabisa kilichokutoa chadema na kukimbilia ccm ni hayo uliyoyataja hapo juu??!ebu ndugu yangu kama kweli unamuogopa MUNGU tuambie ukweli,mimi naishi hapa uk(YORKSHIRE) najua kila kitu ktk nchi yangu hivi wewe kweli ulikuwa hujui ?au kuna kitu nyuma ya pazia?hay bwana karibu nyumbani ila hakikisha GWANDA UNALIRUDISHA KWA WAHUSIKA na sasa UVAE GAMBA RASMI
ReplyDeleteASANTE MDAU UK YORKSHIRE
huyu muachenijamani ana njaa kali.
ReplyDeleteHana aibu anajifanya kukaa majuu kumbe huka hukaa mazuzu pia
inasikitisha kaka umeishi uk muda wote unashindwa kujua nini tofauti ya serikali na chama tawala, ujui wajibu wa dola ni nini, ujui kwanini tunalipa kodi, kweli kaka kukaa ulaya sio kujua kila kitu, pole kwa kutokujua nini kazi za dola na chama tawala
ReplyDeleteHuyu jamaa hayupo Ulaya, Mbona huko maendeleo ni makubwa sana na bado kuna vyama vya upinzani?
ReplyDeleteNi vyema ukawa mkweli tu kwani barabara za lami zilikuwapo Uchagani tangu miaka ya sabini lakini ndio ngome ya upinzani
Kwani wewe unatoka moshi au arusha? Kama hutoki huko ulitegemea kupigiwa simu? Hao ndio wanaijeria wa hapa bongo kama ulikuwa hujuagi.
ReplyDeletehii kali kuliko zote nimecheka hadi basi " ati idadi ya kenge inazidi mamba" hii mupya ha ha haaa! we chris hujatulia.
ReplyDeleteWewe naona unaweweseka tu. Kama hadi sasa huoni mafanikio ya upinzani basi nyamaza kimya:
ReplyDelete(1) CCM imebadilika sana (imeboreka) na hii ni kwa sababu ya upinzani - hasa CHADEMA
(2)Bunge linawajibika zaidi na hii ni kwa sababu ya upinzani - hasa CHADEMA
(3) Kwa sehemu kubwa chachu ya mchakato unaoendelea wa katiba ilianzishwa na upinzani - hasa CHADEMA
(4) Kuhusu maendeleo unayoyasema, je fedha zilizopotea kwa ubadhirifu zingetumika kwenye maendeleo tungekuwa wapi sasa? Kama tungeweza kupiga hatua kwa 100% kwa nini turidhike kwa 40%?
Huu waraka wako onaonesha namna ulivyo mbumbumbu kwenye mambo ya msingi ya siasa (basics)na mimi nakushauri uachane kabisa na uongozi wa siasa usije kuaibika...Uko completely blind kwa mafanikio ya opposition Tanzania. Nakubali wapinzani wana matatizo yao lakini wamefanya (na wanafanya) kazi nzuri. Si unaona hata Mheshimiwa Kikwete kamteua mpinzani (Mbatia) kuwa mbunge? Sasa kama hata Rais na Mwenyekiti wa CCM anaona umuhimu wa upinzani na wewe uko dunia gani ndugu yangu?
Inaonekana wewe hujui siasa za Tanzania kwa hiyo hata huo uongozi wa Chadema usingekufaa. Hao waliokutoa walifanya sawa kabisa. Sababu zako za kujitoa haziendani na mawazo ya KIMAPINDUZI waliyonayo wapinzani. Wewe inaonekana unachukulia siasa kama mambo ya mahusiano ya kubinafsi (kwamba huyu kaja hakunisalimia, nk)...
ReplyDeleteUmeanza vizuri kwenye hii barua yako na katikati ukaanza kubonronga. Nimeacha kusoma katikati. Achana na siasa bro. Utapoteza muda bure.
ReplyDeleteMFANYABIASHARA!!! Wewe ulitegemea maslahi ambayo hukuyapata. Pole sana! SAsa huko CCM unadhani watakuchagua mwenyekiti?? Utasubiria sana.
ReplyDeleteaisee ungekaa kimya kwa miaka kama mitano hivi watu wakusahau, alafu taratibu unaingia CCM, ila sasa portfolio yako haijakaa vizuri;
ReplyDeletekama mwenyekiti wa Kitaifa kwenye nchi iliyoendelea, una political adviser kweli? angekwambia ukae kimya.
ona sasa?
NIKIKUMBUKA NALIA, NIKISAHAU NACHEKA. SIKUJUA KAMA ITAKUWA HIVI.
= = =
Buffalo, New York
Huyu atakuwa amebanwa na kodi mahali. chezea ccm.
ReplyDeleteKatumwa huyo. Yameshindikana amemua kurudi alipotoka.
ReplyDeleteTusichanganye njaa na siasa.
Michuzi usibanie hiyo
Njaa ndo zinasababisha hayo yote...it seems unafuata mkumbo tu maana umeachika chadema ndo umeamua uende CCM!Wamekutema chadema wenyewe kwa kukuona hukidhi vigezo vyao sahv unajifanya kuwa eti unajisafisha ili CCM wakupokeee....
ReplyDeleteKuwa na msimamo acha usiwe malaya wa vyama maana ccm wakikutema sio ajabu utaamia TLP kwa Mrema.
Hapo huna pointi hata moja mmaana barabara zlikuwepo tukea enzi hizo!Eti hujaona barabara nzuri tokea uzaliwe!!!zimejengwa na mapapai nn mkuu?
haahaa!! acha njaa...
i smell a rat! this guy is an OPPORTUNIST.
ReplyDeleteLUKOSI:
ReplyDeleteNakupongeza sana kurejea CCM kwa sababu hizi (5) nzito kabisa,
1.Wewe sio Mchagga hivyo hata ungefanya nini usingedumu hapo.
2.Ungepoteza muda bure kwa kuwa hawa jamaa wananchi wenye akili wameshawashitukia.
3.Hao hao Chadema hawajiamini ktk chama chao kwa kuwa ni kuti kavu linaanguka saa yoyote ile.
4.Chama hicho kimeshapoteza mwelekeo, kimebaki kuhubiri Machafuko, fujo na vurugu
5.Hawajakuwa na utayari wa kuendesha Serikali( INA MAANA HATA KAMA WAKIJARIBIWA KUPEWA MKOA MMOJA TU WATAWALE KAMA NCHI WATASHINDWA),,,MFANO NI MANISPAA YA ARUSHA TOKEA IANGUKIE MIKONONI MWAO UCHUMI WA ARUSHA NA HADHI YA JIJI KWA KASI YA AJABU VIMEPOROMOKA!
mzee chris mimi naona piga boxi tu achana na siasa. Eti Mbowe alikuja uk hata kukusalimia hakukusalimia, sasa wewe ni mkwe au? utajuaje kama alikuja na safari binafsi. Hata aibu huna eti ilikuuma...kubwa zima bwege!! nilikua nakunywa bia zangu umenitoa stimu yote
ReplyDeleteNamnuku "Nikakumbuka msemo mmoja"KWANINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO" MWENYEKITI Mbowe alipita hapa uk lakini mpaka anaondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi(SINA UHAKIKA KAMA ULIKUWA NA RATIBA YAKE)yoyote wa chadema"
ReplyDeleteKaka mimi na maswali kidogo ya kukuuliza je kilichokutoa hasa chadema ni kwasababu ya zile barabara ambazo ullizziona bongo na ambazo hujaziona toka kuzaliwa kwako(SIJUI ZIKOJE HIZO WADAU EMU NIPENI TASWIRA MAANA SIJATIA MGUU NYUMBANI MUDA MREFU KIDOGO) au umejitoa chadema kwa sababu Ndugu Mbowe (UTANISAMEHE NATUMIA NDUGU MAANA MIMI NAAMINI NDIYO UTAMBULISHO MZURI TULIORITHI
TOKA KWA BABU YETU JK NYERERE) alivyopita uk (SIYO KUJA NI KUPITA TU)hakuwasiliana na wewe?maana hiyo Mwenyekiti wa ccm taifa akipita uk au nchi yoyote na ratiba ikambana utahama tena ccm uende chama kingine?, kwa upeo wangu mdogo wa uelewa wewe kuna jambo limekukimbiza huko ,ushauri wangu tuliza akili halafu angalia pa kukanyaga vinginevyo UTAPOTEZA MWELEKEO maana maelezo yako kama unanafasi jaribu kuyapitia vyema "siasa zinawenyewe tusiwe tunakurupuka tu
Asante Mdau Uk Bradford
Mimi nadhani walioandika wengi hapa ni CHADEMA. Mbona mnahasira jamani kwa nini. Mtu kama ameamua kuondoka basi ameamua. Sio lazima muanze kumjadili mpaka mnajichanganya wenyewe
ReplyDelete
ReplyDeleteToka nizaliwe mimi siyo CCM wala Chadema u cha nini?, Mimi ni Mtanzania na hii to tosha, mambo tambarare.
Well what can i say!!!!!!!!!!
ReplyDeleteAkili kweli mali, milembe inakusubiri wewe, CCM hatukuhitaji kwanza wewe sio Mtanzania.
Ulishaukana Utanzania muda mrefu kwa njaa zako eti kuwa mwingereza kutatatua matatizo yako, ukaanznisha biashara ukaomba tenda TBS hukupata ukaamua kusema TBS inaibia watu UK,Ukajiunga CHADEMA baada ya kuwajibika ukaamua kutangaza biashara yako kupitia chama na ukapoteza wateja, Chadema kibarua kimewaka majani baada ya kukushtukia unafanya biashara haramu sasa unarudi CCM, hivi unaakili wewe?
Na ngoja hapo TBS itakapoanza ukaguzi wa mizigo yote ambayo inaingizwa nchini Tanzania kwa x-ray machine, na wakisha yakuta madunguli yako ambayo unatumia wasamaria wema kufanya biashara haramu nathani hapo itakutokea puani.
My advised to you***SHUT UP AND LEAVE POLITCS, YOU CANT PURCHASE CELEBRITY TITLE,THAT BECOME NATURE******
Wewe CCM itakusaidia nini, mheshimiwa Kinana hata hakufahamu wewe, bora ungebaki Chadema tu, ama kweli njaa kali. Nadhani wewe ni mmoja ya walio katiwa Child tax credit sasa unaona maisha magumu huko UK.
ReplyDeleteKama tutaenderea kuwa na watu kama wewe tena wa kutuwakilisha mawazo yetu huko ughaibuni basi taifa letu litaenderea kurudi nyuma. Wakati mwingine kukaa kimya au kutoonyesha misisimamo ya njaa ni nguzo kwa watu wanaokusikiliza, kwa hakika ungekuwa kijijini kwetu hata heshima anayopewa mganga wa kienyeji usingeipata kwani inaonyesha hauna fikla ya manuu ya umma bali ubinafsi. Lest in Peace the First President of the United Republic of Tanzania nitaenderea kukulilia hasa ninapooona hukuwahi kuvaa uniform ya CCM hii inaonyesha jinsi ujamaa na UTU ulivyokuwa na nguvu kwako zaidi ya uchama, uchoyo na ubinafsi. GOD BLESS YOU EVER
ReplyDeleteHao ndio wahafidhina wa CCM ambao hupewa pesa ili waweze kutumiliwa ndugu yangu humdanganyi mtu hapa njaa tuu inakusumbuwa wewe kama umekaa UK kweli uliyoyaona bongo si maendeleo ila ni upuuzi tuu bongo inashindwa hata na BURUNDI nchi ambayo ilikuwa vita vitupu sasa inaitwa swiss ya africa nini unazungumza wewe kama umeishiwa kaa kimya tuu nduguyangu tunajuwa makontena yako yatatolewa free sasa bandarini lakini tutafuatilia na tutahakikisha unalipa ushuru kama wafanyabiashara wengine wowote wale .mimi nilikuona smart kumbe mjinga sana tu wewe any way good luck.
ReplyDeleteWewe wacha propoganda unalako jambo umerudi CCM unajitangazia kwenye ma Blog na ulivyo ondoka ulichana kadi yetu ya chama CCM sasa nani atakupa nyingine? na ukizingatia kashfa na matusi ulitukana chama chetu na viongozi wetu mitandaoni na kuongea na watu unadhani sisi wanachama tunaokujua wa UK tumesahau? kwanza wewe miaka yote umekaa ulaya hujasafiri kurudi kwenu ina maana karatasi zilikuwa hazijatulia nini ? eti ooh nimeona barabara ina maana hata news anatuwekea ankal kila siku za maendeleo ya home na ccm inafanya wewe ulikuwa husomi ? na hiyo kadi wakikupa labda ukachukue makao makuu ya chama tena kwa msamaha mkubwa huko huko bongo kwani sisi UK hata kwenye mikutano ya wanachama hatutaki usogee mana tuna shaka na huu uozo wako labda kaoge bahari saba kwanza. si bure unalo unalolitafuta lakini kumbuka ccm iko imara na makini na hatuli matapishi....ccm oyee
ReplyDeletehehehehehe ama kweli mfa maji haishi kutapatapa , Ankal kwanza huyu jamaa alilewaga thatcha house akakutukana mpaka wewe na kukuzalilisha sana kuwa wewe ni kibaraka wa CCM kwa sababu ulikuwa huweki matangazo ya CCM ,sasa leo anarudi huku amesahau nini huku ?
ReplyDeleteKaka Lukosi
ReplyDeleteUshauri wa bure siasa hazivamiwi siasa zina wenyewe uingie kwenye siasa na heshima kama unavyoingia kanisani sio kama unaharakia choo. Una mdomo mchafu sana wewe kaka naumemtukana sana Mweyekiti wetu wa Taifa eti ooh anasafiri sana ankula hela ya nchi kumbe ilikuwa unakuuma hukupata nafasi ya kusalimiwa nini ndio ukakimbilia huko Chadomo sasa yamekukuta yapi na huko nako Mwenyekiti kapita UK ukakosa salamu , na wakusalimie wewe nani si Misheni town wa kitu haramu hehehehehe...CCM oyeeee na hatukutaki kwani umeona sisi ni fisi wala mizoga we jamaa vipi
Bwana Chillisosi (jina lako la Jamii forum unalotumia kuikashifu CCM na Viongozi wake ) tenda zinakusumbua eeeh? ama kweli baniani mbaya kiatu chake dawa
ReplyDeletewewe lukosi njaa itakumaliza tena acha unafiki ina we miaka yote unarudi tz hizi barabara ulikuwa huzioni ndio umeziona juzi ?unarudi bongo kila mwaka kabla na baada ya kujiunga chadema sasa leo kulikoni au ulikuwa kipofu mwenzetu ? ungetafuta sababu nyingine bana hapa umechemka na CCM chama makini usifikiri baada ya kuandika upuuzi huu ndio watakukaribisha labda umuombe Mzee Mrema anatafuta viongozi kule uanzishe TLP huko UK
ReplyDeleteJamaa kwa kusema kweli...Chadema Wamemfukuza na kumvua uwanachama kama kwamba alijaribu kuingia kunufaika lakini wakamuwahi. Pia mambo yake yamekwama kwa kujiusisha na Chadema. Freight company si yake anawenzie kwa hivyo wenzie wamemwambia kachemsha kafanya company yao kuwa na pingamizi nyingi capitol hill ~(Serikali) dar es salaam kila kitu kinakwama sasa mfamaji kahamua kurudi CCM lakini chama cha mapinduzi tayari wanamjua kama ndumila kuwili watampa kadi lakini mambo yake badoyatakuwa magumu hakuna mtu atakuwa na imani naye.. kama yeye mjanja lazima hawe kimya kwa muda kwani Chadema sasa hivi watamjibu na kusema kila ukweli walio hupata kuhusu yeye...
ReplyDeleteHongera lukosi ulikua umepotea wala usijutie maamuzi yako
ReplyDeleteMhe. Mbowe alipokuja UK hakuona sababu ya kutaka kusalimiana na wewe kwa kuwa tokea anaondoka Tanzania alishaona CV yako na kuwa ktk VIPENGELE MUHIMU KWA CHADEMA NI KABILA , AMEONA WEWE SIO MCHAGGA HIVYO HAKUONA UMUHIMU WA KUONANA NA WEWE HUKO UK!
ReplyDeleteLUKOSI KUWA MAKINI HUKO ULIKO:
ReplyDeleteUmesha kwaruzana na watu wa Mapanga mkononi shaa shaa, hivyo pamoja na ya kuwa upo huko UK kuna Rule of LAW na Polisi huko iko makini sana lakini usikae hivi hivi kwa sababu,
1.Jamaa CDM ya huku TZ wafuasi wao huko UK wanaweza kuwatumia Mapanga kwa njia ya DHL ama EMS Postal despatch mail ili waliopo huko wakukate kawoshi mikono na msikio kwa mapanga!!!.
2.Toa taarifa ya dharula Polisi Uingereza kuhusu uslama wako.
3.Kuwa karibu na Ubalozi wa Tanzania huko UK kwa msaada wa haraka.
Poa umefanya vizur tu bwana Lukosi,siasa zitakukwaza shuguli zako
ReplyDeleteHo Gera kwa kushtuka mapemaa welcome back tunawangoja wengine wote watarudi tu no tension
ReplyDelete