Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe Gaudencia Kabaka (kushoto), akimkabidhi kombe, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi katika Benki ya CRDB, Esther Kitoka, baada ya benki hiyo kushika nafasi ya pili, katika hafla ya utopaji tuzo za Mwajiri Bora Tanzania 2012 zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog) 
 Baadhi ya maofisa wa CRDB wakiwa katika hafla utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2012

 Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na tuzo tatu walizoshinda katika hafla ya utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora.

BENKI ya CRDB imejishindia tuzo tatu ikiwamo ya Fedha kwa kushika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2012, zilizohusisha zaidi ya Kampuni 30, ambayo ilipokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa benki hiyo Esther Kitoka.

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) , ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

Akiongea wakati wa kukabidhi tuzo hizo, Rais Kikwete, aliwashukuru waajiri Wakitanzania, mashirika ya umma na binafsi kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kuisadia Serikali kutengeneza ajira na maendeleo ya uchumi na pia alikiri uwepo wa tatizo la ajira hapa nchini.

“Ninayo furaha kushiriki nanyi jioni ya leo. Mmekuwa msaada mkubwa kwa taifa letu na ninapenda kuwaahidi kuwa Serikali itawasaidia katika shughuli zenu,” alisema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete aliongeza kuwa, juhudi za Serikali pekee haziwezi kuifanya nchi ya Tanzania kuwa yenye kipato cha kati labda kama kutakuwa na juhudi kati ya Serikali na sekta binafsi ambazo zitasaidia  kupunguza idadi ya Watanzania wasio na ajira nchini.

Rais Kikwete ametoa changamoto kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Serikali kufanya kazi kwa pamoja katika masuala mawili muhimu ambayo ni maendeleo ya rasilimali watu hasa katika uendelezaji wa ushirikiano wa maendeleo kati ya taasisi za vyuo vya juu na viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...