Tafadhali mwanangu naomba unibandikie mawazo/ushauri wangu kwa jamii wachangie kuhusu masikitiko ya asilimia 56 ya watoto wa Lindi wana utapiamlo.Ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye mtandao.Ni mzee na ninaomba wazee wenzangu tuendelee kujitokeza kujiunga kwenye mtandao katika kuchangia mawazo yao kwa Taifa na itakuwa ni changa moto kwa vijana wetu wa dot.com wazee wenye mawazo ya hekima wamo lakini hawavumi. Asante nategemea ushauri wako kwa ombi langu na kunisaidia kulisahihisha na kulitoa kwa jamii kama linafaa,maana wewe ni mzoefu wa matangazo. Nakutakia kazi njema mwanangu. Mdau Amai Kimaro

Nasikitika kusoma Gazeti la Mtanzania la Dec.12.2012 asilimia 56 ya watoto wa Lindi wana utapiamlo.Naomba jamani turudi nyuma tulikotoka wazazi wenu.Kuna Idara ya Maendeleo ya Jamii ni mojawapo wa kazi zao kuelimisha na kushauri jamii kuhusiana na tatizo/shughuli husika za kiamaendeleo.Watoto kwanzia Mwezi 0-mpaka Miaka 5 wanatakiwa uangalizi wa hali ya juu kiafya.Zamani mama maendeleo walikuwa wa
nafundisha kina mama kutengeneza vyakula vya watoto wapofikia miezi ya kula mpaka kufikia miaka 5,ambapo anaweza kula vyakula vya wakubwa.Na walikuwa wanafundisha kutokana na vyakula wanavyolima wenywe.
Mama maendeleo walikuwa wanashirikana na wauguzi wa Clinic kufanya home visiting kila kwa wiki mara moja .Kufanya hivyo ilikuwa inasaidia sana kugundua matatizo yanayoikabili jamii na kutafuta njia ya kuyatatua ikiwa moja wapo kutoa ripoti kwa wahusika.
Naiomba Serikali iangalie umuhimu wa Idara hii ya Maendeleo ya Jamii kwa kuwapa vitendea kazi kuwafikia jamii kwa urahisi wasikae Maofisini tu huku jamii inaumia.Ikumbukwe mupo k wa ajili yao na ndiyo hasa majukumu yenu. Kama kweli yaliyo andikwa watoto 56 wana utapiamlo ni aibu kwa Taifa kama kuna njaa jamani SERIKALI iwaangalie iwasaidie vyakula vya virutubisho kuokoa hawa watoto ambao ni nguvu kazi ya TAIFA Naomba jamii tuchangie kutoa ushauri.

Mdau Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. WEWE ULIOTOA MADA BASI WASADIE.

    ReplyDelete
  2. Assalam Alaykum,

    Masheikh na Manwinyi wa Lindi, malezi ya watoto yanategemea Wazazi kwa lishe na mipango ya masomo na mengineyo.

    Tatizo kubwa ktk jamii zetu kwa ujumla, ni kujali zaidi kuongeza idadi ya wake licha ya kuwa kitendo hiki ni sehemu ya Uumini lakini ni mujibu kuangalia pia uwezo na hali kama tayari ktk familia pana watoto, malezi ya watoto kwa lishe na hatima ya masomo ni muhimu pia na vya kupewa kipaumbele!!!

    ReplyDelete
  3. Sawa idadi zaidi ya wake ni sehemu ya Uumini.

    Licha ya hilo, Mamwinyi Lindi acheni kuongeza wake zaidi mjali kwanza malezi ya watoto LISHE+MASOMO !

    ReplyDelete
  4. MAMWINYI LINDI,

    ONGEZENI IDADI YA WAKE KWA UWEZO KIHALI UKIWEPO!

    WACHANENI NA NDOA ZA MITAALA (WAKE WENGI) HUKU UWEZO WA MALEZI UKIWA CHINI KUWEZA KUTOA CHAKULA CHA UHAKIKA NA BORA KWA WATOTO.

    ReplyDelete
  5. Hii inatokana na ile hulka ya kupenda kuoa bila kuzingatia uwezo!

    Imekuwa ni Lindi kumekithiri hali hiyo, unaweza kuona hali hii huko Kilimanajaro au Kagera kitu kama hiyo ?

    ReplyDelete
  6. Utafiti unatumia sampuli na si idadi halisi ya watu. Hakuna taasisi iliyopima watoto wote wa Lindi na kupata takwimu hizi. Haya ni majumuisho tu ya kitafiti.

    ReplyDelete
  7. UUMINI UNATUSISITIZIA TUISHI KWA KUMTEGEMEA MWENYEZI NA PIA TUWE NA MIPANGO YETU KIBINAADAMU.

    RIZIKI ANATOA MWENYEZI.

    1.HAIKATAZWI KUZAA WATOTO WENGI AMA KUWA NA WAKE WENGI, TUANGALIE NA UWEZO PIA, HILI HATA KATIKA MIONGOZO YA KIIMANI TUMEWEKEWA.

    2.NDANI YA MIONGOZO YA KIIMANI, TUNASISITIZWA KUZINGATIA MALEZI YA FAMILIA ZETU WAKE NA WATOTO KWA MATUNZO, CHAKULA NA HUDUMA KUWAJALI NA UPENDO UKIWA SEHEMU YAKE PIA.

    3.HIVYO ISICHUKULIWE KUZAA BILA BREKI AMA KUONGEZA IDADI YA WAKE BILA MIPANGO NA UTARATIBU NI SEHEMU YA IMANI.

    ReplyDelete
  8. Nyumba za Ibada Lindi kazi hiyo mmeiona?

    ...Jukumu la kuwalisha watoto kuwaokoa kwa utapiamlo...

    Isiwe mnapitisha kofia kila baada ya Kipindi cha Ibada halafu zooote zinazama kwenye mifuko ya makoti ya Viongozi wa Kiimani!

    ReplyDelete
  9. Mambo mliyosema hapo juu kuhusu mitala ni kweli kwa jamii nyingine za Tanzania. Kumbukeni kuwa Lindi watoto ni mali ya mama kwa hiyo ni jukumu la wajomba kulea watoto. Labda mfumo mzima wa jamii ubadilike. Halafu kwa jamii nyingi tu mama ndiye huwa anajitahidi kujenga ustawi wa familia. Badala ya kulaumu umwinyi, nadhani tutilie mkazo elimu ya jamii kwa akina mama. Nunua chakula cha ntoto ( utani hapo) kabla ya kununua kanga na mikufu ya dhahabu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...