Ni video nyingine kutoka Visual Lab. Kama lilivyo jina la wimbo,kupitia video hii, Professor Jay anaweka bayana hali mbalimbali za kimaisha na matokeo yake.Kuna kupanda na kuna kushuka.
Usimdharau mwenzako asiyenazo hii leo kwa sababu hujui kesho utakuwa wapi na katika hali gani.Yote anapanga Muumba.
Pia Profesa Jay anakemea sio tu hali hiyo bali pia hata kitu ambacho kwa mapana na marefu kiliitia doa nchi yetu.
Ni kitendo cha baadhi ya binadamu kuwageuza wengine kuwa “dili”.Kitendo cha wapuuzi fulani kuwaua albino kwa imani potofu kabisa za kishirikina na kupata utajiri.Itizame video hii na kisha usisite kutoa tathimini yako.
Yaani katika aina ya muziki ninaoudharau ni huu hapa. I really don't see the beauty ya bongo fleva, huu si muziki wetu kwanini mnang'ang'ania kuuita wa kwetu?
ReplyDelete