Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nana kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi.
vijana wa Klabu za Jogging 12 za maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam wakishiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Iddi Azzani akiongoza timu yake ya Klabu ya Jogging ya Barafu ya Magomeni wakati wakishangilia ushindi wao.
"Hapa lazima waje..." Mh. Iddi Azzan akishiriki kuvuta kamba.
Iddi Azzani Akizindua bonanza hilo kwa kupiga penati golini.
Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya Jogging ya Kawe na kuondolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hali ya hewa haikuwachenjia kweli?

    ReplyDelete
  2. bongo bwana mchezo ni kuvuta kamba au kufukuza kuku... chezeni walao volleyball au wekeni mziki muachie sebene la nguvu hayo ndo yatakuwa mazoezi ya ukweli mwili wote unafurahi, na siyo kuvuta mikamba kila leo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...