Meneja Uhusiano wa kampuni ya Vodacom-Tanzania, Matina Nkurlu (Wapili kushoto), akimuelekeza mmoja wa waandishi habari, jinsi ya kununua bidhaa kwa kutumia huduma ya M-Pesa, kwenye duka la Shoppers, Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kampuni ya vodacom kwa kuanzia imeanza kutoa huduma ya kununua bidhaa kwa kutumia M-Pesa kwenye maduka ya Shoppers ya Msasani na Masaki, yote ya jijini.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Vodacom-Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia), akichagua bidhaa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza Dar es Salaam. Waandishi wa habari walifika kwenye duka hilo , kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia huduma ya M-Pesa.
Mpigapicha Mkuu wa Kampuni ya Free Media Group, inayochapisha gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, (katikati) pamoja na Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Fidelis Felix (kushoto)wakilipia bidhaa zao kwa njia ya M-Pesa walizozinunua ndani ya duka la Shopaz Plaza Msasani. Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya TSN, inayochapisha magazeti ya Dailynews na HabariLeo, Robert Okanda, akinunua bidhaa kadhaa ndani ya duka la Shopaz Plaza Msasani ambazo alizilipia kwa kupitia huduma ya M-pesa, Kampuni ya vodacom kwa kuanzia imeanza kutoa huduma ya kununua bidhaa kwa kutumia M-Pesa kwenye maduka ya Shoppers ya Msasani na Masaki, yote ya jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu , akiwaelekeza waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza namna huduma ya M-Pesa inavyotumika kwa manunuzi ya bidhaa ndani ya duka hilo. Waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini walifika dukani hapo kupata mahitaji mbalimbali na kulipa kwa kutumia huduma ya M-pesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...