Mwanamuziki kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akitia saini moja ya bango lenye kampeni inayowatahadharisha madereva wa magari kunywa pombe kupindukia,ikiwa ni hatari kwa afya na usalama wao kwa ujumla,pichani kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Steve Gannon akishuhudia tukio hilo,aidha katika tukio hilo Wanahabari mbalimbali walishuhudia tukio hilo ndani ya hotel ya Serena Inn mapema leo mchana.Koffi Olomide na skwadi lake la Quartie Latin wametua jana jijini Dar kwa ajili ya maonesho yao mawili yatakayofanyika jijini Dar ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni siku ya jumamosi na jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM-Kirumba siku ya jumapili kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya SBL kupitia bia yake ya Tusker Lager.
 Bango alilotia wino Koffi Olomide.
 Koffi Olomide akitoa vionjo vya moja ya wimbo wake mbele ya wanahabari,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano Serengeti Breweries,Nandi Mwiyombela akinogesha
Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru akiuzumguza mbele ya Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Inn,kuhusiana na onesho la Mwanamuziki kutoka DRC-Congo,Koffi Olomide linalotarajiwa kufanyika kesho jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar. Picha zaidi BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Watu watumie usafiri wa teksi na wa umma baada ya kunywa bia na siyo kungangania waendeshe magari yao ili kuepuka ajali kutokana na ulevi.
    Mdau
    Ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...