MFUKO
wa Taifa wa Taifa wa Afya (NHIF) kesho unazindua rasmi mpango wa huduma
za bima ya afya kwa vikundi vya wajasiriamali ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
Mama Salma Kikwete.
Uzinduzi
huo utafungua milango kwa vikundi mbalimbali kujiunga na huduma za
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) tofauti na ilivyokuwa hapo awali
ambapo wafanyakazi wa Sekta rasmi tu ndio walipewa nafasi ya kutumia
huduma hizo.
Kwa
mujibu wa Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa
NHIF, inasema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja kuanzia saa 2.30 asubuhi.
Taarifa
hiyo imesema kwamba uzinduzi wa mpango huo unatoa fursa kubwa kwa
Watanzania kuhakikisha wanaingia kwenye utaratibu wa bima ya afya ili
wawe na uhakika wa kupata matibabu.
“Hii
ni fursa nyingine ambayo Mfuko imeona iitoe kwa Watanzania na hii
inatokana na ukweli kwamba huduma za matibabu zimekuwa zikipanda kila
kukicha na wananchi wengi kushindwa kumudu gharama hizo na wakati
mwingine kusababisha madhara makubwa yakiwemo ya kupoteza maisha…mtu
akiwa kwenye utaratibu wa bima anakuwa na uhakika wa kupata matibabu
wakati wowote hata kama hana fedha mfukoni,” ilisema sehemu ya taarifa
hiyo.
Shughuli
kubwa zitakazofanyika katika uzinduzi huo ni pamoja na kuzindua huduma
hiyo, kugawa vitambulisho vya matibabu kwa wanachama wapya ambao
wamejiunga kupitia vikundi vya wajasiriamali vinavyoratibiwa na WAMA.
Sina kingine mie, ila huyu mama mzuri.
ReplyDelete