Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akitoa amri ya kuifunga hotel ya Double Tree kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Karim Kanji - Mkurugenzi Mkazi wa hotel hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa (wa kwanza kulia) akikagua mfumo wa maji taka katika Hotel ya Double Tree jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwana na Dkt. Robert Ntakamulenga kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Na Lulu Mussa na Ali Meja

Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameifungia hotel ya Double Tree ya Jijini Dar es Salaam kutokana na kutiririsha maji taka baharini.

Waziri Huvisa ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Charles Kitwanga.

Ziara hiyo ililenga kuona utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa awali na Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga mapema mwezi huu, alipofanya ziara kutembelea viwanda na hoteli zilizo pembezoni mwa bahari kuona mfumo wa maji taka.

Katika ziara hiyo, Hotel ya Double Tree iliagizwa kuwa na mpango wa muda mfupi na wa haraka wa kusitisha utiririshaji wa maji taka baharini ambao mpaka leo hotel hiyo ilikuwa bado haijatekeleza.

Sambamba na hilo na hilo Waziri Huvisa amefuta hati ya ukaguzi wa Mazingira (Environemental Audit) na kuitaka hoteli hiyo kurekebisha mara moja mfumo huo ikiwa ni sambamba na kulipa faini kwa baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Hotel ya Double tree iiliyofungiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, kutokana na kutiririsha maji taka baharini. Hotel hiyo imefungwa hii leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. ule mfereji pale ocean road unaoingia bahari ni wa tiririsha maji machafu naomba nao pia ufungwe ili kunusuru mazingira.
    Mdau
    muogeleaji pwani ya Ocean road

    ReplyDelete
  2. NYIE VIPI?MNAPOKEA DOLA ZA WATU HUKU MNAWAPA MAJI YA CHUMVI?

    ReplyDelete
  3. JAMANI AJIRA ZA WATU ITAKUWAJE?MUNGU TUSAIDIE WANAO.By Sopphy.

    ReplyDelete
  4. Ili silielewi, wafanyakazi wake wako wapi mpaka Waziri aje afanye kazi hii? Naomba mnieleweshe tu.

    ReplyDelete
  5. Hoteli hii inajina kubwa sana!

    ''DOUBLE TREE by HILTON''

    Lakini kwa sababu Karata ni ya Jokeri yaani mwendeshaji Mhindi mbana matumizi na mkwepa Kodi anaendesha kwa jina la Leseni ndio maana unakuta vitu kama kutiririsha maji taka!

    Kama wangeendesha wenye Jina wenyewe wasingefanya upuuzi huu!

    ReplyDelete
  6. Sasa yatiririke wapi?

    ReplyDelete
  7. Inaonesha jamaa aliwashindwa hao wanume wenzie akaenda kumleta Mama. Big woman hakuna mchezo funga zote

    ReplyDelete
  8. Huu ni uonevu tu, inaonyesha huyo waziri ana chuki binafsi. kibomba hicho ndio cha kuchafua mazingira si kweli. Inasikitisha muwekezaji atoe rushwa ili aendelee na biashara. Kwa njia hii hatutafika.

    ReplyDelete
  9. Hongera Mama Huvisa. Kaza buti hao ni kati ya wengi wanaochafua mazingira kwa aina hiyo... Wapo wengine wengi huku mikoani Uje napo Uwafungie - wawakilishi wako wanapepesa tu... Moshi hapa tuna mradi wa maji taka - wakatiflani Mji unanuka kinyesi... Vipo viwanda vya ngozi na amasoko na wadau wa samaki.... uchafu na uharibifu mtupu!!

    ReplyDelete
  10. Sasa maji machafu yasipoenda baharini yaende wapi? Maji ya choo yote ya mjini yanaingia baharini sasa nini tatizo? Au watu wamenyimwa rushwa?

    Michezo hiyo tunaijuwa longtime watu wakinyimwa rushwa huwa wanafungia biashara za watu

    Hiyo ndio tanzania a.k.a bongo bana

    ReplyDelete
  11. Hawa ndio Wawekezaji wenyewe hata Mashariti na kanuni za afya ni mgogoro hawavifuati!

    Itakuwa Kodi watalipa vizuri?

    ReplyDelete
  12. Hivyo mazingira machafu kwa hoteli fanyeni india lakini sio TANZANIA!

    ReplyDelete
  13. Its the infrastucture problem which is managed by the city. The hotel has nothing to do with this problem. The whole city has no sewer system where do think the waste go? Waziri hilo sio jibu kufungia hotel jengeni sewer system kwani hata Ikulu haina sewer system nayo utaifungia?
    Bongo tambarare.....

    ReplyDelete
  14. Mnataka hayo maji taka yapelekwe wapi? kwani mmejenga bwawa la kuyatiririsha? Mbona hilo ni tatizo sehemu nyingi sana kwanini Double Tree Hotel tu? au kuna kanjaa kanawasumbua?

    ReplyDelete
  15. Anon wa kwanza.
    YA OCEAN ROAD NI BY DESIGN, UNAKWENDA KUYAMWAGA MAJITAKA KWENYE KINA KIREFU SANA SIO UFUKWENI. BAADA YA HAPO YANACHUKULIWA NA MKONDO. SIO SAWA NA HUU MFUMO WA HIYO HOTELI AMBAPO MAJITAKA YANAKWENDA UFUKWENI.

    ReplyDelete
  16. kwa bongo yetu hapa lazima kuna jambo. Nilivyomuona Kitwanga last week katinga ghafla bin vuu nikajua hapa jamaa wa Dabo Mti kuna sehemu wametibua. Leo hii mpaka mama wa vikao, makongamano na semina nae kaingia mtaani basi kweli kuna jambo na hii stori ya maji taka ni kuzuga tu!!

    ReplyDelete
  17. Hii haitoshi kufungia tu taasisi hizi ni fimbo ndogo sana, inabidi kuwatoza faini juu ya uchafuzi wao, natoa pondezi hata hivyo juu ya hatua iliyochukuliwa na serikali. Kaka michuzi huna budi nawe kupata chochote juu ya hizi pongezi kwani kuwatangaza hawa waharibifu wa mazingira ni moja kati ya silaha ya kuboresha mazingira.

    ReplyDelete
  18. Imefungiwa leo, na Kesho itafunguliwa.

    Tunaomba utoe NEWS ALERT KWAMBA
    HOTEL YA DOUBLE TREE SASA YAFUNGULIWA.

    Mfanyakazi wa Double Tree

    ReplyDelete
  19. Ferry soko la samaki la kimataifa hapo Kigamboni, Dar-es-Salaam napo panahitaji waziri afike maana kila kitu kinafagiliwa na kutupwa bahari ikiwemo maji machafu ya soko la samaki.

    Pia kuhusu bomba la Ocean Road baharini hili nalo katika dunia ya sasa halitakiwi kutiririsha maji kina kirefu au kifupi au ufukweni. Maji-taka yanatakiwa kushugulikiwa (kuwa-treated) kwanza kabla bomba la maji machafu la Ocean road kumwaga maji-taka kina kirefu baharini.

    Suala hapa liwe ni sheria na kiwango(standard) moja kwa kila mkaazi, taasisi, biashara, soko n.k walio na makaazi jijini Dar.

    Waziri wa mazingira na Halmashauri ya Jiji la Dar inatakiwa wasiende kwa kuchagua wapi sheria ifuatwe na wapi isifuatwe.
    Mdau
    Kigamboni

    ReplyDelete
  20. Hivi kweli huyu mama nae miaka mitatu hoteli ipo kwenye operation leo ndio anasema hoteli inachafua mazingira tunajua doubletree wamegoma kutoa rushwa na hoteli zote za mwambao wa baharini zinamwaga maji yake machafu baharini na wametoa rushwa kwa kitwana.

    ReplyDelete
  21. Mkadarasi hakujuwa haya? wakaguzi majengo whawakuyaona haya? HAO wanamazibgira hamkuyaona haya mapema mpaka jengo linatumika?....acheni roho mbaya wewee!

    ReplyDelete
  22. Nina wasiwasi 10% hapa haijatembea, mbona zipo nyingi sana zinachafua mazingira huku upande wa mikocheni na Upanga?

    ReplyDelete
  23. Hapa dar watu wengi wanajenga mamansion lakini wanajenga makaro nyumba lya nyumba kwa sababu hakuna sewer system, mimi niliomba sewer system kutoka dawasco basi kuunganisha ni 7,000,000/= na nyumba ya mtaani high density. inapata nyumba 7 hivi kutoka chamber kuu. Sasa hoteli bila ya shaka wamewatoza nyingi na rushwa juu. Halafu wale wafanyakazi wa dawasco wanasema tutakufanyia sisi kwa milioni 2,000,000 lakini at your own risk.

    ReplyDelete
  24. jamani na ile ya agakhan iangaliwe, maana hadi sindano na vinyesi vipo jujujuu, ni hatari kwa kweli.

    ReplyDelete
  25. Mtafuteni Profesa Manyele wa UDSM awafundishe namna ya kudhibiti mfumo mzima wa taka na mazingira katika mji. Wataalam tunao kila uchao kazi kupiga makelele. Imefikia wakati sasa watu wafanye kazi kwa kuzingatia na kuheshimu taaluma na mipaka ya kazi za watu siasa ziwekwe kando.

    ReplyDelete
  26. Come on and stop the nonsense... Your guests have been complaining about the smell which comes from how you chose to get rid of the wastes for a long while and you did nothing about it.

    Just google "DoubleTree Tanzania Sewerage"... To quote one of your guests "Firstly the smell from the bay... Sewerage is the word that comes to mind, which ruins the beautiful setting, the pool and bar area ..."

    It always amazes me how some of these folks come to do business in Tanzania and decide to blatantly break the law. What they did on the coastline, they would not be able to do it in many of the other countries they operate. Such a shame! And now they claim to be working with the Ministry of Environment, where were you? Finally you got caught... Bribes only gets you so far...

    ReplyDelete
  27. Tunahitaji mpango kazi wa muda mrefu katika majiji,manispaa na miji ya Tanzania ili iwepo fomula moja elekezi kwa wadau wote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...