HABARI ZIMETUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA KWAMBA MBUNGE WA ZAMANI WA TABORA MJINI SIRAJU JUMA KABOYONGA  (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA GHAFLA SAA NNE USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

KWA MUJIBU WA TAARIFA KUTOKA NSSF, AMBAKO ALIWAHI KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MFUKO HUO WA JAMII, MAREHEMU KABOYONGA ANATARAJIWA KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI NA MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE SINZA, JIJINI DAR ES SALAAM.

MAREHEMU PIA ALIWAHI KUWA KUWA MENEJA WA KANDA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN DEVELOPMENT BANK - EADB) KATIKA OFISI ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM.

TUTAENDELEA KUWAPA TAARIFA ZAIDI KADRI ZITAKAVYOTUFIKIA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Inalillah wainna ilaih swabirinna

    Marehemu pia alifanyakazi Benki kuu ya Tanzania kwa nyazidhifa mbalimbali.

    Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.Amina

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Aamen

    ReplyDelete
  3. Habari hii inasikitisha sana jamani. Such a good and unique brain is gone!! Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu. Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.

    Nawatakia Familia yake wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu. POLENI SANA.

    ReplyDelete
  4. So sad Mungu awape moyo Wa subra Pole sana ndugu yangu issa

    ReplyDelete
  5. Inna lillahi wa inna ilaihi rajiun. Very unique, smart, talented individual. I have soo much respect for the man, should have made a good Governor. Salam zangu za rambi rambi zimfikie Issa, Musa na Fatma Siraju pamoja na ndugu na jamaa wa marehemu. Mungu amlaze peponi. Your help will always be remembered

    ReplyDelete
  6. Mungu ailaze roho ya mpiganaji wetu mahala pema peponi!

    ReplyDelete
  7. Mohamed Siraju KaboyongaJanuary 06, 2013

    mungu ailaze roho ya baba yangu mpendwa mahala pema peponi...we'r loving u so much daddy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...