Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro
Na Peter Mwenda
MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa na kundi lake la Tanzania One Theatre (TOT) leo kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala, jijini Dar es salaam kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.
Akizungumza jana, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kinatamba na nyimbo kemkem za taarab zinazotingisha katika miondoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake katika eneo hilo kwenye sikukuu hiyo.
Alisema TOT taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.
Mkurugenzi wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakaocheza taarab vizuri na watakaovaa vizuri.
Alisema burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambapo Januari 29, 2013 bendi ya Msondo Ngoma itatoa burudani katika ukumbi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...