Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Event Limited Bw Rena Calist akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Seaescape iliyoko Mbezi Afrikana jijini Dar es salaam wakati akizungumzia matayarisho ya mwisho kabla ya shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika kesho Desema 21 kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.Katika shindano hilo wanashiriki warembo kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na na baadhi ya nchi jirani na ukanda h ambapo mshindi wa shindano hilo anatarajiwa kujinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za Kimarekani elfu thelathini 30,000.Kushoto ni Guetano Kagwa ambaye atakuwa MC wa shindano hilo na kulia ni Serge Nkurunzinza Mwakilishi wa Miss East Africa nchini Burundi .
Guetano Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kulia ni Rena Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. "Dondola angalia sana kiuno kitakatika"

    ReplyDelete
  2. Natabiri burundi wataibuka washindi ktk mpambano huu.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa tatu unatabiri Burundi?

    Hebu angalia picha ya 3 kutoka juu hao wawili kutoka kulia wa pili na wa tatu, utakuja kusema baada ya Mashindano, Eti nini Burundi?,,,mwanawane kazi ipo Rwanda na Eritrea !

    ReplyDelete
  4. Ohhh wewe mdau wa pili hapo juu unaema Burundi?, hujamwona dada yake Niyonzima wa Kigali-Rwanda hapo?

    ReplyDelete
  5. Ahhh!,

    Hawa wasichana wetu wa nywele za Manyoya ya farasi kweli wapo hapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...