MzeeYusuf akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live usiku wa 'Boxing Day'.
Mke wa Mzee Yusuf, Leila Rashid, akizikonga nyoyo za wapenzi wa taarab usiku wa kuamkia leo.
Khadja Yusuf akiwachizisha wapenzi wa taarab ndani ya Dar Live.
Mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab, Fatma Mahmoud 'Mcharuko' akiwapa raha mashabiki.
Nyomi iliyohudhuria shoo hiyo kali kutoka Jahazi Modern Taarab.
Mzee Yusuf akiongea na mashabiki wake.
...Khadja Yusuf kazini.
Bi. Leila Rashid akiendeleza makamuzi.
Mzee Yusuf akizidi kukoleza burudani ndani ya Dar Live.
Wapenzi wa taarab wakijiachia kwa raha zao na Jahazi.
Sehemu ya nyomi iliyotia timu mahali hapo.
---
Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake, Mzee Yusuf ' Mfalme' usiku wa 'Boxing Day' lilifanya makamuzi ya nguvu ndani ya ukumbi wa maraha wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kuzikonga nyoyo za wapenzi wa taarab waliofurika mahali hapo. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyochukia nafasi wakati wa shoo hiyo.
(PICHA: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jana nilifunga safari kwenda kushangaa hii Dar live.Show hii ilikuwa nzuri,ukumbi mzuri,huduma nzuri.Mahudhurio 60% akina Dada na 40% akina Kaka.Kinachoendelea humo ukumbini siyo taarabu tu(Tafakari).Ni balaa.

    David V

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu kwa kuangalia picha hapo juu mimi naona wanaume ni 80% na wasiochana ni 20%. Haya ni mapinduzi ya kuhuzunisha katika Taarabu.

    ReplyDelete
  3. HEEE DAVID V, umerudi eeh kwa umekuja holiday eeh? nitakusakane eb michu muweke huyu mdau humu tumuone ukute tushapishana naye maeneo bilakujua, nahamu yakumjua kaswaaaaaa kama baraka wa chibiriti.

    ReplyDelete
  4. Yeah nimekuja holiday Dar(Kwetu kuzuri),napata tabu sana na joto la Daresalaam.Na siyo joto kusema kweli-Ni humidity(Unyevu?).Unyevunyevu upo juu sana Daresalaam kipindi hiki.Tutakutana tu bado nipo hadi katikati ya January 2013.Nawatakieni wote heri ya mwaka mpya 2013

    Hilo kundi linalocheza hapo ni asilimia 10 tu ya watu wote waliokuwemo ukumbini.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...