Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wajumbe wa semina elekezi ya madiwani wa CCM wa Mkoa wa Rukwa wakati akifunga semina hiyo iliyoanza jana na kumalizika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. 

Kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete. Semina hiyo iliyokuwa ya mafunzo ilikuwa na lengo la kuimarisha utendaji kazi wa chama hicho pamoja na kukiongezea chama uwezo zaidi wa kuisimamia shughuli za Serikali katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama hicho pamoja kukiongezea nguvu zaidi kiweze kushinda katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015.

Semina hiyo ilikuwa na jumla ya mada tisa amabazo ni historia ya CCM tangu TANU na ASP, Katiba ya CCM ya mwaka 1977-2012, Sera za msingi za CCM, Muelekeo wa Sera za CCM mwaka 2010-2020, Sera za Umma, Utekelezaji wa sera Ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea katika mazingira ya utandawazi na uchumi wa soko, Hali ya kisiasa na mikakati wa ushindi kwa ajili ya uchaguzi Mkuu 2015, Uandishi wa katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na Majukumu yatokanayo na taarifa ya kazi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM 2012.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete akizungumza kwenye ufunguzi wa semina hiyo jana. Katika maneno yake ya ufunguzi alisema lengo kuu la semina hiyo ni kuimarisha chama kiweze kushika dola kwa kutatua kero zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisema Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake bila ya msukumo kutoka katika chama, aliwataka viongozi katika ngazi zote kuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli za maendeleo badala kukaa tu ofisini na kuagiza walio chini yao.
Kiongozi wa wakufunzi wa semina hiyo Ndugu Lukasi Kisasi akijitambulisha kwa wajumbe wa semina hiyo.
Baadhi ya madiwani waliohudhuria semina hiyo wakiskiliza kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo, jumla ya madiwani 64 wameshiriki kwenye semina hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza katika Semina hiyo. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...