Asalam Walyekum Kaka Michuzi!
Naamini kwa uwezo wake rabuka unaendeleza jahazi letu salama!
kaka juzi tar 17 nimetoka kukuandikia jinsi gani kilimanjaro na arusha tunalea wahalifu, usiku nikiwa naangalia taarifa ya habari ya ITV (unaweza pia angalia youtube)
mkoani Arusha- Namanga wamekamatwa wahabeshi 98 wakiwa wanasafirishwa kwenye fuso kuelekea mkoani Mbeya!
Sasa cha kusikitisha ni kwamba mmoja wa utingo aliekamatwa jina lake la mwisho ni sawa na yule utingo aliekamatwa mwaka jana desemba Morogoro na wahabeshi 98 ambae kwasasa anatumikia kifungo chake. waliohukumiwa ni dereva na utingo tu!
Hii ya juzi aliekua anawaelekeza njia alipohojiwa alisema kuna "tajiri'" alimpa hela kwa nia ya yeye kuwaonyesha njia maana yeye ni mwenyeji, jamani sio kwa nia ya uchonganishi ila huyu kinara amekua akitumia ndugu zake ambao wanaishia kufungwa wakati yeye akitafuta nyoka wengine.
Kaka haya ni mapambano,Rais alishatangaza vita na wahamiaji haramu maana iko siku tutapigwa bomu tuishie kulia,hivi unadhan ndugu zao wanafurahia hii hali,jamani tuweni makini maana tunakoelekea ni kubaya.
Tukemee maovu kabla ya hatari. Huyu kinara wao ambae naamini uhamiaji wana taarifa zake akamatwe achukuliwe hatua.
mdau
KWA HALI ILIPOFIKIA KWA SASA:
ReplyDeleteRUSHWA NA ULAJI NCHINI,
AENDE MAWAZIRI WENYEWE WAHUSIKA WA WIZARA HIYO KUWAKAMATA HAO VIGOGO BADALA YA MAAFISA WA UHAMIAJI AMBAO WANGALI WANAJENGA NYUMBA ZAO HAWATAWEZA KUWA NA MBAVU ZA KUKABILIANA NA WAZITO WANAOGAWA NOTI ZA KIGENI ($$$$$$) KAMA HAWA MATAJIRI WA SAFARI HARAMU.
MFANO, TUMESHUHUDIA WAZIRI MHE. HUVISA TEREZYA JUZI NA JANA AKIENDA MWENYEWE KUWAKAMATA NA KUWAFUNGIA BOUBLE TREE HOTELS KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWA KUTIRIRISHA MAJI TAKA HOVYO!
Acheni roho mbaya hizo. Hao Wahabeshi hawaji TZ wanaenda zao SA kutafuta maisha sawa na Wabongo wanaokwenda UK, USA, EU kuhangaika na maisha.
ReplyDeleteni kweli kabisa mdau,mimi nakaa kilimanjaro na ni kweli kuna kifaru mmoja tunaishi nae na anahusika na hii biashara haramu. mi nachojua pesa inanunua kila kitu,huyu mtu kukamatwa ni hadi bahari ikauke.
ReplyDeleteKwanza niwaambie ukweli, mtandao wa kuingiza hawa wahabeshi nchini UHAMIAJI nao wapo ktk mtandao huu kwa asilimia 100 nina uhakika huu!
ReplyDeleteNi ndugu zetu tunakaa nao na sio siri huwa wanajisahau na kupayuka!
Tena hadi Maafisa wakuu wa Mikoa ya K'njaro na Arusha ni washiriki wakubwa wa 'biashara' hii.
Wewe unaesema waachwe utakuwa hujuhi ubaya wa biashara hii haramu ya human traficking...nilikuwa kama wewe mwanzoni...mpaka nilipobahatika kuangalia movie moja imechezwa ulaya Mashariki nililia machozi...watu wanafanyiwa ndivyo sivyo na hawa wasafirishaji...mabinti wa miaka 18 and below waliishia kujiuza bila malipo wakati walikuwa promised kupelekwa Italy na wazazi japo walipinga mwanzo walilainishwa na promises kibao za hawa so called agents wa u model only to end up being (forced)prostitutes, na watumia madawa sugu and the movie was based on true story; mtandao wa wafanya biashara za watu ni mgumu sana kuu control hata Ulaya...we tema mate chini...unajua South Africa wanachoenda kufanya au kufanyiwa???????? unajuaje kama hawa jamaa hawawaui wakifika mbele na kusafirisha viungo vya binadamu ambavyo ni very marketable????
ReplyDelete