Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwa katika gazeti la Mwananchi la Desemba 24, 2012 akiwa amevaa sare za JWTZ.

Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askari wa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli.

 Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa (jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. 

Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kama ni sare halisi ya JWTZ. Ilikuwa rahisi kumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. 

Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwi kujihusisha katika masuala ya kisiasa.

 Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo.

 JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu. 

 Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 
 Makao Makuu ya Jeshi, Upanga 

 SLP 9203, 
Simu: 0764 742161 
 Email:ulinzimagazine@yahoo.co. uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Makao makuu ya Jeshi mnatumia email za yahoo.?Na hamna Landline hadi mtumie hiyo Mobile?.Kila la kheri

    David V

    ReplyDelete
  2. MWANAJESHI MWENYEWE MBONA KAMA WA KWENYE ZE KOMEDI

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa kama kweli ni mwanajeshi basi ni mwehu.

    ReplyDelete
  4. Eti kafunika uso, kwani vyote huwa munaonesha uso?

    ReplyDelete
  5. Jeshi msitake kujisafisha kwani wengi wa wapiganaji wenu hawana taaluma na uelewa wa kutosha na pia jeshi lina matabaka makubwa na siku ikijakuwa wazi basi kila mtu atashika mdomo wake na kustaajabu.Nasikitishwa na afisa uhusiano kutoka upanga kuzikana uniform za jeshi wakati hivi majuzi tu nimewaona jwtz hao kule kambi za kigoma wakiwa na hayo mavazi tena chakavu.Hebu tuwe wazalendo na tuache ubabe usio na maantiki wafundisheni katiba na maadili wapiganaji wenu sio kuwaonea tu huku nyie mkiwa mmekaa mkizunguka na viti ma ofisini na huku mkitafuta umaarufu.Hao ndio mtawategemea baadae kwenda Malawi sijui na wapi.Be honest...by msemakweli

    ReplyDelete
  6. Msimlaumu mwanajeshi, huyo mbunge wetu wa Arusha anaelekea kuwa hata sheria hajua naona ushindi umempunguzia hata uelewa wa mipaka ya furaha yake. Jeshi wa chadema huyo. CHADEMA hawana jema na hii nchi hata kidogo Kama jeshi linagawanywa kichama basi 2015 tutaenda kujificha jirani Malawi. Nchi haitakalika kama wanavyosema.

    ReplyDelete
  7. Hao Chadema wanataka kutupeleka pabaya.

    ReplyDelete
  8. Go to hell JWTZ nyinyi hamshiriki Siasa wakati dunia nzima sio takwimu Za TZ tu hadi watu weupe wanajua kuwa CCM inasaidiwa na vikosi vya ulinzi kwa kila kitu,POLISi -jESHI NYOTE MNATUMWA NA CCM NA WALA SIO SERIKALI

    ReplyDelete
  9. Hivi sasa Chadema mnaacha kuvaa makaki na mnaingia kwenye hizi camouflage za wanajeshi?

    ReplyDelete
  10. Wa kukamatwa ni Uongozi wa Chadema hasa huko Monduli na huyo huyo Lema ili wataje ni yule ni nani na anatokea Kikosi gani?

    KWISHA!!!

    Hatuwezi kulea Uasi nchini Tanzania, haya mambo ni ya huko Mashariki ya Kongo na Rwanda, hapa Tanzania hapana!

    ReplyDelete
  11. LEMA ANATAKIWA BADALA YA KUNYA'NGANYWA UBUNGE SAFARI HII AZAME LUPANGO KABISA KWA KUSAIDIA UASI WA KIJESHI NCHINI!

    ReplyDelete
  12. HAHAHA YANI NILIVYOONA PICHA YA HUYU MWANAJESHI KWENYE GAZETI LA MWANACHI NILICHEKA SANA NIKASEMA KWELI MAKAMANDA WA CHADEMA NI WAJANJA KWELI YANI WAKAMFANYA MWANAJESHI FALA NAE ASIJUE MIPAKA YA KAZI YAKE JAMANI SIASA NI GAME MOJA HATARI SANA ILA MIMI SIAMINI KAMA HUYU NI MWANAJESHI WA UKWELI AU NI WA KUPANDIZA NINI KAMA VILE MTU WA CCM ANAVALISHWA GWANDA ALAFU ANAFANYA FUJO MAHALI WANASEMA ALIKUWQA MTU WA CHADEMA

    ReplyDelete
  13. Poleni,
    Sawa ni mwanajeshi, yeye amepiga picha na mtu, si chama cha siasa wala bendera ya chama. Sasa kuna kosa gani.

    Ijue sioni cha kumfukuza kazi, mimi naona tu ni kuwaelimisha tu,ili wawe makini wanajeshi.

    Mkifukuza akienda mahakamani atawashinda tu. Lema na mtu si chadema.

    ReplyDelete
  14. hivi hii ni kweli email ya yahoo? huu utani sasa utatofautishaje? Nipeni kazi jamani msilazimishe fani IT hamna hapo.

    ReplyDelete
  15. Yaani ktk maoni yoote niliyoyasoma ni mtu mmoja tu ndie aliyetoa maoni yaliyopevuka kifikra nae ni huyu wa: tue dec25, 08.02 pm 2012.
    Ashitakiwe kwa kupiga picha na huyo mbunge?wanauthibitisho wowote zaidi ya hiyo picha kwamba anajishughulisha na siasa? kuna baya lolote hapa lenye maslai ya taifa zaidi ya hofu na woga binafsi dhidi ya kilichopelekea tukio hili? nadhani wakati muafaka wa kunukuu hivi vipengele vilivyonukuliwa hapa na hii hamasa ya kutaka kumbaini huyu askari ni inapotokea kuwa askari jeshi wamepiga raia,wamepiga trafiki,wamevamia baa na kumwaga vinywaji,wamehusishwa na ugomvi wa kugombea mwanamke, vitu ambavyo kiukweli mara kwa mara vinatokea lakini huwa vinatawaliwa na ukimya kana kwamba hakuna lililotokea.Nadhani kuna haja ya kuliangalia hili suala kibusara zaidi kuliko kukurupuka hasa ktk ulimwengu huu wa watu wenye kumbukumbu nzuri.

    ReplyDelete
  16. Binafsi yangu sioni kama kuna tatizo ,kama alivyosema jamaa hapo juu kwani kupiga picha na kiongozi wa kisiasa si kosa,mbona kuna matukio mengi tu ya maafisa wa jeshi la wananchi kupiga picha na viongozi wa wakuu wa kisiasa ,mimi ningepata tabu sana kama huyo mwanajeshi angepiga picha ameshika kadi ya chadema hapo sawa ,lakini picha si kigezo cha kuwa unamuunga mkono mwanasiasa muhusika au chama cha kisiasa,Natumai jeshi letu litatumia hekima zaidi ktk kushulikia swala hili
    Asanteni

    ReplyDelete
  17. Kwani jamani mnaosema picha haina ishara yote ya kisiasa hivyo atawashinda and blah blah angalieni ishara ya chadema aliyoionesha pale...msisumbuke kushabikia siasa ni mchezo mchafu nyie waachieni wenyewe..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...