Baraza
la sanaa la taifa limeteua majina matatu ya wabunifu wa mavazi nchini
Tanzania kuwa waamuzi wa shindano la wanamitindo bora wa mwaka wenye
sifa za kipekee nchini Tanzania (Unique Model 2012).
Uteuzi
wa majaji hawa umezingatia sifa za cv za majaji sita zilizowakilishwa
baraza la sanaa la taifa na hatima yake yakarudi majina matatu ambayo ni
Asia Idarous,Gymkhana Hilall (paka wear) na Martin Kadinda.
Fainali
za unique model 2012 zinafanyika ijumaa ya wiki hii tarehe 28 Desemba
katika kumbi la maraha ulioko kule Oysterbay yaani naongelea New
Maisha club ambapo wanamitindo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.
Burudani
ya bendi mahili katika muziki dansi,Mashujaa band ikiongozwa na Chalz
Baba watatoa burudani kali kwa mashabiki watakaohudhulia fainali hizo
siku ya Ijumaa hii.
pia
msanii B-shop kwa mara ya kwanza ataonekana jukwaani. Ikiambatana na
mashamushamu ya Costa siboka na burudani ya wanamuziki mbalimbali kwa
kiingilio cha Tsh 15,000 tu.
Shindano hili
limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa
investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la
Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments
& Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na
Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design,Dina ismail blog na Unique
Entertainment Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...