RUBANI wa ndege ndogo mali ya TANAPA, Athuman Bujwanga (47) mkazi wa Mahale Kigoma amenusurika kifo baada ndege hiyo aliyokuwa akiiendesha kupata hitilafu ikiwa hewani na kuanguka kando ya Mto Nsemulwa nje ya mji wa Mpanda Mkoani Katavi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo .
Alisema kuwa ndege hiyo aina ya Cessna yenye uwezo wa kubeba abiria wanne yenye namba za usajiri 5H F25C 182 ilianguka umbali wa kilometa moja kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda uliopo Kashaulili muda mfupi baada ya kupaa, ikiwa njiani kuelekea Mlele katika mbuga ya Taifa ya Katavi kujaza mafuta.
Ndege hiyo ilifika Mpanda ikiwa na abiria mmoja ikitokea Tabora na kisha baada ya kumshusha abiria huyo iliruka kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kujaza mafuta ili iweze kurejea Tabora.
Mmoja wa walio shuhudi tukio hilo Credo Mwanisenga, alieleza kuwa wakati akiwa anafanya shughuli zake za kilimo ghafla aliona ndege iliyo kuwa angani ikizimika na kisha baada ya muda mfupi ikaanguka jirani na mti wa mwembe. Mara, walifika katika eneo hilo kwa lengo la kutoa msaada. Iliwachukuwa muda kuanza kutoa msaada kwa rubani huyo aliyekuwa ndani ya ndege peke yake, kutokana na eneo hilo kuwa na nyuki wengi ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao.
Hata hivyo waliewza kufanikiwa kumtoa rubani huyo huku akiwa amepata majeruhi makubwa sehemu ya uso wake na maumivu sehemu ya kifua hali akikohoa damu. , rubani huyo alipewa msaada na wananchi waliokuwa wakifanya shughuli zao za kilimo kwenye mashamba yao karibu na eneo ilikotokea ajali, na alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya mjini Mpanda kwa gari la Meneja wa Uwanja wa Ndege aliyefika kwenye eneo la tukio, ambapo alishondwa nyuzi nane katika paji lake la uso na hatimaye aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Naye Meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda, Mahamud Muhamed alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 10 na dakika 55 jioni katika kijiji cha Nsemlwa wilayani hapo.
Ndege hiyo imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
Muhamed alisema taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha ajari hiyo kilitokana na njini ya ndege hiyo kufeli wakati ikiwa angani, hata hivyo uchunguzi wa kina kuhusiana na ajali hiyo bado unaendelea.
picha kwa hisani ya KATAVI YETU BLOG
Hivi vindege vidogo mbona vinapata hajali sana...mi nlishahapa kuwa sivipandi hata kwa mtutu
ReplyDeleteMwenyezi amsaidie Rubani!
ReplyDeleteKutoka Uwanja wa ndege angani hadi aridhini katikati ya shamba la mahindi?