Nani kakwambia Tanzania muziki wa kizazi kipya ni Bongo Fleva pekee?? Cheki watasha wanavyochenguka na Mchiriku live wa Jagwa Music toka Mwananyamala jijini Dar es salaam katika Roskilde Festival nchini Denmark mwaka jana. Achaaaaa!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hawa ndio wakombozi watu kwa sisi watu ambao tunaishi mbali na jumbani,sema cha kushangaza zaidi ziara zao za ulaya blog ya jamii aiweki wala ratiba yoa,wakati utumbo wa kajumulo kila siku tunauona ktk blog,watendeeni haki kidogo wana jagwa kwani uku ulaya wanaheshimika sana,nakumbuka mwaka huu walifunika jiji la nijmegen nl

    ReplyDelete
  2. Jamaa wametulia sana. Siye wabongo wa Ughaibuni tunasema wakati wote kwamba,wenyeji wa huku na sisi tunataka utamaduni wa kweli. Wasanii wakija wawe wanavaa Kiafrica au wanaimba Kiswahili na Lugha za kikabila. Lakini Wabongo tumekuwa mbogo tunajifanya tunajua (kwahiyo tuna kaa kimya). Na Anony. wa 1siyo lazima kumkashifu mwenzio (Kajumulo)kwani angalua anajaribu kufanya kitu cha maendeleo. Na kusema kweli simfahamu Kajumulo lakini jamaa ana juhudi ya kuitangaza Tanzania sana. Tuache chuki binafsi.

    ReplyDelete
  3. msimsagie Kajumulo, yeye Babu Kaju ni mtumiaji wa TEHAMA na hivyo hawa kina Jagwa na wadhamini wao pia wachangamkie TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

    Pia nawashauri JAGWA na wadhamini wao waitumie GLOBU YA Jamii maana ina mtandao dunia nzima na inaweza kuwasaidia ktk harakati zao za kufanya muziki-asilia kujulikana kwa nguvu zaidi na kasi zaidi.
    Mdau
    JK

    ReplyDelete
  4. Michuzi muziki wetu wa asili ni pamoja na huu ila si bongo fleva. Fleva ni ujinga tu wala hauna ubunifu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...