Atlantic Star wamepiga vibao kibao ila ngoma ya Silver shadow ilipagawisha sana katikati ya miaka ya 80

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 'Sugar so Honey' hii ni kete nyingine tamu sana ya hawa Atlantic Star ilipigwa miaka ya 1981-82 hivi kama sikosei.

    Wadau toeni uhondo, ahhh zamani kulikuwa kutamu jamani tuache utani!

    Sio hivi sasa mabalaa kama haya chini:

    1.mifumuko ya bei na kupanda kila kukicha gharama za maisha.

    2.mia ya mmasai ya noti nyekundu ilikuwa ni pesa, lakini kwa sasa maajabu ya mussa tunakuta LAKI SI PESA!!! ,,,(wakati mia ya noti nyekundu ikiwa pesa ina maana laki itakuwa ni kama Bilioni au trilioni lakini ahhh wapi)

    3.migogoro na chuki baina ya watu

    4.visukari na presha ilikuwa ni magonjwa ya matajiri lakini sasa tunachangia wote masikini na wenye nazo, kubwa lao tuna mgogoro wa miwaya kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa hakuna, watu walikuwa wanakwenda pekupeku lakini sasa inabidi watu watumie kinga kwanza.

    5.maadili yameporomoka, unazaa mwana wewe unakuwa ndio mtoto na mwana anakuwa ndiye mzazi wako!!!,,,unapewa amri tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...