Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, hukwadau mbalimbali wa masuala ya mapambano yA ukimwi wakishiriki kwa kufanya maonyesho na kutoa elimu na maelezo mbalimbali yanayohusu mapambano ya ukimwi, Rais Pia ameshuhudia utiwaji saini wa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 308 kutoka mfuko wa Global Fund uliosainiwa kati ya Katibu katibu wa Ofisi ya rais Paniel Lyimo na Ramadhan Kijahkatikabu Mkuu Wizara ya Fedha huku Mfuko wa Global Fund ukiwakilishwa na Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko huo.
Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko Global Fund akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo . kutoka kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Hussein Mwinyi, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS,Fatuma Mrisho.
Rais Jakaya Kikwete akishuhudia Utiwaji wa Saini wa msaada wa dola za Kimarekani milioni 308 kwa ajili ya mapambano ya Ukimwi nchini, mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Paniel Lyimo kushoto na Ramadhan Kijah katikati, kulia ni Christoph Benn mkurugenzi wa Mfuko wa Global Fund, waliosimama nyuma kushoto ni Mkewa Rasi Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Ursula Muller Mjumbe wa bodi ya The Global Fund,
Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi tayari kwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo yamefanyika mkoani Lindi kitaifa.kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS Fatma Mrisho na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...