Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula (pili kulia) akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda(pili kushoto) msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh milioni 10/- kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindano ya kuwania Kombe la Meya wa Kinondoni 'Kinondoni Mayor Cup 2012" katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Naibu Meya kinondoni Songoro Mnyonge(Kushoto) na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo Sharif Maji.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula (kulia) akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda (kati) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10/- kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Meya wa Kinondoni, Dar es Salaam. akishuhudia ni Naibu Meya kinondoni Songoro Mnyonge.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula (kati) pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda (kushoto) na Naibu Meya kinondoni Songoro Mnyonge wakiwa na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 10/- vilivyokabidhiwa na Benki ya NMB.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...