Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini na Serikali ya Wilaya ya Mvomero alipowasili Mtibwa - Madizini, Turiani huku akiongozwa na Askofu Godfrey Sehaba , wa Dayosisi ya Morogoro, kabla ya kuanza kwa ibada ya kuombea hafla ya harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Stefano eneo la Mazini , Turiani ambayo ilifanyika Desemba mosi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka na Askofu ni Mkuu Askofu Godfrey Sehaba .
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akizungumza na waumini wa Kanisa la Anglikana wa Mtibwa , Turiani pamoja na wananchi wengine walioshiriki ibada maalumu ya harambee ya uchangiaji ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Stefano - Madizini.wapili kutoka kushoto ni Askofu Godfrey Sehaba wa Kanisa hilo Dayosisi ya Morogoro na wapili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (kulia) akizungumza machache wakati akitangaza kuchangia fedha yeye binafsi na sambamba na uongozi wa Wilaya na pia kuwakilisha Mkoa wakati wa harambee ya uchangiaji ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Stefano - Madizini,Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro uliofanyika Desemba mosi mwaka huu.Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa na Kushoto ni Askofu Godfrey Sehaba wa Dayosisi ya Morogoro Kanisa la Anglikana.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( wa kwanza kulia) kuchangia fedha yeye binafsi na sambamba na uongozi wa Wilaya na pia kuwakilisha Mkoa wakati wa harambee ya uchangiaji ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Stefano - Madizini uliofanyika Desemba misi mwaka huu , Madizini ( kushoto) ni Askofu Godfrey Sehaba wa Dayosisi ya Morogoro Kanisa la Anglikana,
( Picha na John Nditi).


Pesa ni zao waweza kuzitumia wapendavyo. Nami ni mcha Mungu, lakini nafurahi zaidi nikiona michango ya kujenga hospitali na shule, siyo makanisa na misikiti
ReplyDeleteKweli mdau wa kwanza,nadhani ktk afrika yawezekana nigeria ndio nchi ya kwanza kua na idadi ya nyumba za ibada na nikijaribu kupata picha ya kinachotokea kule napata kidhungudhungu.Bora shule, hospitali na barabara za vijiji.
ReplyDeletehayo maoni yako! nami nayaheshimu! lakini si vibaya tukawapa watu nafasi na uhuru wa kufanya vile mioyo yao ilivyopenda! wakijenga misikiti na makanisa nayo ni huduma ya jamii! ni uhitaji umekuwepo, wakaamua kujitolea kufanya! mambo ya kufanya yapo mengi zaidi ya tunavyoweza kufikiri!
ReplyDelete