Mhe.Balozi  Rajabu Gamaha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia) na Balozi Albert Shingiro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi wakiweka saini barua ya pamoja kwa niaba ya Serikali ya Nchi zao ambayo itawasilishwa kwenye Shirika la Kijerumani la GIZ ili kuomba msaada wa kuimarisha mpaka kati ya Tanzania na Burundi.
Balozi Gamaha kulia akibadilishana mawazo na Balozi Shingiro mara baada ya zoezi la uwekaji saini barua kukamilika.
Ujumbe wa Serikali ya Burundi uliofuatana na Balozi Shingiro ukifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Gamaha na Balozi Shingiro ambao hawapo pichani. Picha na mpiganaji Ally Kondo wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hili ni jambo jema,lakini,nikiunganisha hapa,napenda nitoe ushauri wangu kwa Viongozi wa Nchi zote za Tanzania,Burundi,Rwanda,Congo DRC na Uganda,kupitia blog hii muhimu ambayo naamini wanaisoma mara kwa mara,na ushauri wenyewe ni huu:"Ili kulimaliza "kabisa" tatizo au mgogoro huu wa mipaka na usalama wake,kati ya Congo DRC na majirani zake,hususan Rwanda na Uganda,Viongozi wa nchi zote hizo nilizo zitaja,WAKAE PAMOJA,kwa maana ya kuitisha Mkutano wa pamoja,ili kuzungumzia UWEZEKANO WA KUZIUNGANISHA NCHI HIZI KWA KUJENGA RELI ITAKAYO YAUNGANISHA MAJIJI YETU MAWILI YA Dar es salaam NA Kinshasa!I know,to some this may sound a crazy idea,but its not,I can assure you!Tayari,Reli ipo kati ya Dar es salaam na Kigoma.Sina uhakika,kutoka Kinshasa kurudi Goma au mpaka wa Ziwa Tanganyika,kama kuna Reli yoyote,au iliyopo imekomea wapi!Kwa hiyo,naweza kusema,Nusu ya Tatizo hilo ni kama limesha pata ufumbuzi.Kilichobaki sasa ni kwa nchi zote husika kuunganisha nguvu ili kuangalia,kipande hicho kilicho salia,Reli itapita katika Miji gani,kuanzia Kigoma,ndani ya Burundi au Rwanda na kuelekea Goma hadi Kinshasa.Uwezo wa kutekeleza Mradi huo upo.These said countries have so much enormous Resource Potential!Kuwepo kwa mradi huo,kutamaliza kabisa Tension iliyopo ya mipaka baina ya nchi hizo.Tukumbuke mipaka iliyopo sasa iliwekwa na Wakoloni (1884) kwa manufaa yao binafsi,na kamwe si kwa maslahi ya nchi za Afrika.Wakati umefika sasa,kwa Viongozi wa Nchi huru za Afrika,kuiangalia Upya dhana hii ya Mipaka ya Wakoloni.Kwamfano,kwetu sisi Watanzania,badala ya "kupoteza muda wetu kulumbana kuhusu Zanzibar iwe hivi au vile,tuelekeze nguvu zetu zote katika kufikiria mambo ya maana zaidi,ya kuiunganisha Tanzania na DRC Congo kwa kuzishirikisha nchi zote majirani,Rwanda,Burundi na Uganda".Najua ni Project kubwa sana ambayo haiwezi kukamilika kesho au ndani ya miaka mitano.Lakini,iwapo Rais Kikwete,ataweza kuwa na uthubutu ,japo wa kujaribu tu,wazo hili lifanikiwe,I can assure you,atakuwa ameacha kumbukumbu kubwa mno ambayo haito sahaulika barani Afrika.Ni kama ukombozi wa kusini mwa afrika phase 2!God Bless Africa! (tonny)

    ReplyDelete
  2. Migogoro ya mipaka isiyoisha zaidi sana baina ya Rwanda,Burundi,na EASTERN Congo DRC,inatokana na "tension inayozikabili nchi hizi majirani zetu na ndugu zetu,za Rwanda na Burundi" kutokana na "Udogo wa Nchi hizo" ki ardhi,ikilinganishwa na kasi ya ongezeko la watu katika nchi hizo mbili(rapid population growth vis a vis limited and scarce land resource area)!Kama nchi zetu za Maziwa Makuu,Tanzania ikishika usukani kama kawaida au Jadi Yetu,katika kusuluhisha migogoro ya kidugu kama hiyo,zikiamua kulitatua tatizo hilo,once and for all,inawezekana kabisa!Tusipumbazwe na hii Mipaka iliyowekwa 1884 ili "kutudhoofisha kwa kutugawa na kutuchonganisha sisi wenyewe kwa wenyewe"!Lets all sit down together and look for a lasting solution for a lasting and enduring peace!Inawezekana kabisa.Tufikirie kwanza,kama vile mipaka baina ya Tanzania na Burundi na Rwanda na Congo DRC,na kwa kule north kati ya Uganda na Congo DRC,mipaka iliyopo sasa "kama vile haipo(as if current geographical boundaries do not exist at all).Kilichopo ni mipaka ya kisiasa tu (political boundaries).Which means,watu wetu wa mipakani mwa nchi hizo "wawe huru kuvuka na kufanya biashara baina ya pande zinazopakana bila ya kikwazo(kutumia majeshi na polisi au immigration,na kadhalika)Kila raia wa nchi mojawapo,mradi tu awe na kitambulisho halali cha utambulisho cha nchi husika,kitakacho kubalika na nchi zote Zinazopakana!Nchi zote zitanufaika zaidi,watu wetu watanufaika zaidi,na uhasama utapungua baina ya raia wa pande zote mbili,na baina ya serikali za nchi majirani.Tukiondoa hiyo tension inayowakabili ndugu zetu wa "land locked tiny countries without adequate arable land resource but with huge population increase",matatizo yote haya yatapungua sana.Tutabakiwa na matatizo madogo madogo ya "njaa ya tumbo" basi!Tanzania,should start doing the social engeneering!Hapa tuna viongozi wenye upeo na uwezo bro!Seriously,hatujijui tu,lakini kwa hili,Watanzania tumebahatika sana.Thanx to Mwalimu Julius Nyerere,Forever and Ever.....(jo)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...