Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA FC) kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jana jioni, ambapo timu ya TASWA FC ilichezea kichapo cha magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaofanyika leo kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambao umefunguliwa na Mdau wa Michezo,Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.
Hiki ndicho kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day (kulia) na Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo,Mh. Ahmed Kipozi (wa pili kulia) akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar Said Salim huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC,Juma Pinto (kushoto) akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Shafii Dauda (kushoto) akimiliki mpira huku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
Mshauri wa timu ya TASWA FC,Masoud Sanani akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...